Wananchi wameshauriwa kutunza vyakula kwaajili ya matumizi ya familia zao ili kujiepusha na madhara ya njaa yanayoweza kujitokeza kutokana na wananchi hao kuuza mazao mengi ukizingatia na uzalishaji haukuwa mkubwa kutokana na hali ya hewa.
Ushauri huu umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija katika kikao cha tathmini ya lishe kilichofanyika leo April 14,2025 ambapo amewaelekeza watendaji wa kata kwenda kuwahamasisha wananchi kuacha kuuza mazao yote waliyovuna badala yake watunze akiba kwaajili ya matumizi ya familia zao
"Kawambieni wananchi wasiuze vyakula vyote watunze akiba, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haina shamba harafu ni aibu kwa Mwananchi wa Kwimba kulia njaa wakati chakula kimepatikana hatakama hali ya hewa haikuwa nzuri sana lakini bado chakula kilichopatikana kisiuzwe chote harafu wakaanza kuhangaika" amesema Ludigija
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewasisitiza watendaji kuendelea kusimamia upatikanaji wa chakula shuleni ili wanafunzi wote wapate chakula " tunataka wanafunzi wote wapate chakula shuleni ili tutengeneze kizazi chenye nguvu, na uwezo wa kufikiri hatutaki kuwa na watoto wenye utapuamlo" Ludigija
Aidha amemtaka Afisa elimu Sekondari kuongeza usimamizi katika Shule ya Sekondari Nyamilama ambayo imeonekana kuwa na wanafunzi wengi, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora na wanakaa katika mazingira salama na wezeshi kujifunza
Akiwasilisha taarifa za Lishe Mratibu wa Lishe Bi. Emma Kalolo amesema Halmashauri inaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwalisha watoto chakula kinachozingatia makundi yote ya vyakula ili kuondoa tatizo la utapiamlo na kuwahimiza wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.