• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Wananchi washiriki sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani

Posted on: March 9th, 2017


Wananchi wa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza wameshiriki sherehe za Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 08/03/2017 ikiwa na kauli  mbiu “ Tanzania  ya viwanda  wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi”

Madhimisho yameanzia viwanja vya Halmashauri kupitia viunga mbalimbali vya mji wa Ngudu hadi  viwanja vya mpira wa miguu KWIDECO na kupokelewa na mgeni rasmi ndugu Andrea Ng’wani kwa niaba ya mkuu wa wilaya.

"Mnaombwa kukemea na kuacha vitendo vya kuwazuia watoto wa kike wasipate elimu ili kuwaozesha. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano imeweka mpango wa makusudi kabisa  katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya msingi na kuendelea hasa mtoto wa kike, na ina kaulimbiu inayosema Elimu bure, hivyo kila mtoto apelekwe shule kwa wakati na asikatizwe masomo yake kwa sababu zisizokuwa na msingi, ikiwemo kuwaozesha katika umri mdogo na kuwafanya walezi wa familia. Serikali ipo makini katika kuzuia mdondoko wa watoto wa kike shuleni na kupambana na mimba za utotoni”

Hayo yamesemwa na Ndg Andrea Ng`wani katibu Tawala wa Wilaya kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya kwimba wakati akiwahutubia wananchi  na amesisitiza  kwa kusema

Mzazi yeyote au Jamii itakayohusika kwa namna yoyote ile kumkatiza mtoto wa kike masomo Sheria itachukua mkondo wake.

 Wakati wa akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Bibi Getrude Nokingile  amesema Wanawake wengi hasa wazee na vikongwe waishio vijiji wanaishi pekee yao na wanaishi katika mazingira hatarishi,ambayo yanawafanya waonekane tofauti na watu wengine na baadhi ya watu kuhisi kwamba kutokana na hali duni ya maisha wanayoishi ni wachawi, ndio wanaosababisha vifo vya watu katika maeneo wanayoishi.Tunaomba serikali kuanzia ngazi ya kitongoji hadi ngazi ya Wilaya kushirikiana na wananchi katika kuwatambua na kuwalinda ili waishi kwa usalama na  amani.

Mwanamke ni mlezi wa familia, ni msingi wa maendeleo na ni kiongozi shupavu wa famililia hayo yamesemwa na Ndugu Innocent Sililo mkazi wa mtaa wa chamhela wilayani kwimba wakati wa  sherehe hizo.

Aidha Bibi Sobi Masalu mamaye ni mkuu wa Kitengo cha Sayansi kimu  Idara ya Elimu Msingi amesisitiza kuwa ili mwanamke aweze kukidhi kauli mbiu ya mwaka huu anahitaji Elimu ya ujasiliamali, Mtaji, mfumo dume kuondolewa, stadi za ujuzi mbalimbali na hasa za maendeleo zifundishwe kwa msisitizo  kuanzia madarasa ya chini na somo la S/Kimu lirudishwe shule za msingi ili mtoto anapomaliza elimu ya msingi awe na maarifa ya kumwezesha kupambana na mazingira yanayomzunguka.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa kuwapa vyeti walimu wa kike kumi  katika shule za Msingi na Sekondari wilayani humo ambao  wamefaulisha vizuri mitihani ya Taifa 2016/2017.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.