Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Duniani kwa kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi juu ya umuhimu wa haki za watoto na umuhi.u wa kuzuia ukatili.
Akiongea na wananchi walioshiriki maadhimisho hayo katika viwanja vya Shule ya Msingi Malya Ndugu Alex Patrick Mwananzyungu Afisa Tarafa ya Ibindo amesisitiza wananchi wote kuhakikisha wanalinda haki za watoto huku akisisitiza kila mtoto kupata elimu.
Aidha amesisitiza wananchi kuzingatia haki za watoto bila kubagua " kutokana na kauli mbiu inayosema HAKI ZA MTOTO : TULIPOTOKA, TULIPO NA TUENDAKO nawasisitiza wazazi na jamii kwa ujumla kutambua umuhimu wa haki za watoto bila ubaguzi " amesema Alex
Amesisitiza kuwa watoto wenye mahitaji maalumu wana haki ya kupata elimu,kupendwa na kupewa ushirikiano kama watoto wengine.
Mgeni huyo amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kupambana na ukati wa watoto hasa kwa kuhakikisha wanapata elimu, na kudhibiti ndoa za utotoni,na kuzuia mila zinazokandamiza watoto
Alex amewataka wananchi wote kuwa mabalozi kuhakikisha wanazuia ukatili kwa watoto, kwa kuhakikisha wanaelimisha na kutoa taarifa wanapoona dalili za ukatili.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Hamza Kibesela akihitimisha maadhimisho hayo amewataka watoto wote walioshiriki maadhimisho hayo kwenda kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na mgeni rasmi pamoja na wataalamu wengine.