Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka Wananchi kutumia kamati ya ushauri wa kisheria katika kutatua kero na malalamiko dhidi ya Serikali na malalamiko kati ya mtu na mtu.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo April 22,2025 kwenye uzinduzi wa kamati ya ushauri wa kisheria ambayo ameizindua rasmi huku akisisitiza kamati hiyo kwenda kutatua Malalamiko ya Wananchi ili kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani na kuondoa malalmiko ya wananchi dhidi ya Serikali
" Lengo kuu la Serikali kuanzisha Kamati hii ni kuwapunguzia kero na malalamiko hasa yanayolenga Serikali lakini na yanayowalenga wananchi wenyewe, kwahiyo niwaombe wote mlioshiriki hapa mkawe mabalozi kuwahamasisha wananchi kutumia kamati hii kutatua changamoto zao"
Aidha ametumia wasaa huo kuilitambulisha dawati la msaada wa kisheria ambalo linafanya kazi chini ya kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia " pia hapa tuna watu wanaofanya kazi kwenye dawati la msaada wa kisheria watumieni" Ludigija
Akiwasilisha taarifa fupi ya kazi Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Helen Chuma Wakili wa Serikali amesema kamati hiyo itakuwa na majuku mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa malalamiko kwa wananchi dhidi ya Serikali, kutoa elimu na kuhamasisha swala la haki na wajibu
" kamati itapokea malalamiko yenye uhalisia wa kile kinacholalamikiwa" amesema Helen
Wajumbe walioshiriki uzinduzi huo wameipongeza Serikali kwa kuanzisha kamati hiyo na wameshauri kamati ifanye kazi kwa kuanza na changamoto za wazi hasa kero ya ajari zinazosababishwa na waendesha pikipiki wasiozingatia sheria za usalama barabarani
" Mkuu wa polisi (W) Kwimba tunaomba aongeze jitihada za usalama barabarani ili hawa waendesha pikipiki wasimamiwe ajari zinaongezeka tunazika watu kwaajili ya ajari za pikipiki hili limetuchosha" amesema Julias Nyerere Mwenyekiti wa Chama cha walemavu
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutatua kero na changamoto za wananchi kwa kuanzisha dawati la msaada wa kisheria na kamati ya msaada wa kisheria ambapo wote wanalenga kumsaidia mwananchi kupata haki na kutatua changamoto bila kutumia gharama kubwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.