Serikali imedhamiria kuondoa tatizo la Saratani kwa wanawake,kundi kubwa la wanawake wamejitokeza katika hospitali ya Ngudu na Kituo cha Afya Mwamashimba Wilayani Kwimba kupima Saratani ya mlango wa kizazi leo tarehe 24/11/2020.
Katika zoezi hilo Mtaalamu kutoka Wizara ya Afya Kitengo cha Mama na Mtoto Bi. Basilisa Sedrick Mdonde amesema Serikali inalenga kuwapima wanawake wote Nchi nzima japo Wizara imeanza na Mikoa miwili tu baada ya hapo wataendelea na Mikoa mingine. Bi Basilisa amesema Saratani ya Mlango wa kizazi ni Saratani inayoongoza kwa vifo vingi vya wanawake hapa Tanzania hivyo utaratibu wa kupima utasaidia kupunguza vifo hivyo kwani Saratani hii ikigundurika mapema inatibika.
Bi. Basilisa Sedrick Mdonde ( kulia) na Ms.Joan Chamungu ( kushoto)
Vilevile katika zoezi hilo alikuwepo Ms.Joan Chamungu Mkurugenzi wa TNW(Tanzania Network of Women Living With HIV/AIDS ameeleza kuwa matibabu ya Saratani ya Mlango wa kizazi hutolewa kulingana na hatua za ugonjwa na hali ya mgonjwa.Amesema huduma za matibabu hutolewa kwa njia ya upasuaji katika hatua za mwanzo za ugonjwa,mionzi,Dawa za Saratani au mionzi na dawa kwa pamoja.Vilevile amesisitiza kuwa wanawake wanapoona dalili zifuatazo:- kutokwa na damu baada ya kujamiana,kutokwa na uchafu sehemu za siri,kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya,kutokwa na usaha sehemu za siri,kutokwa na damu sehemu za siri isiyo na hedhi,maumivu ya kiuno na maumivu ya tumbo chini ya kitovu wawahi Hospitali kwani hizo ni dalili za Saratani ya Mlango wa kizazi.
Wanawake waliojitokeza kupima wameshauliwa kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo kwa kutojamiana na wanaume wengi kwani kirusi cha ugonjwa huo kinasambaa kwa njia ya kujamiana na mtu mwenye kirusi hicho, hivyo wanawake wameshauliwa kupenda na kulinda Afya zao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.