Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Sumve Bi. Rozalia Magoti akitoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazoongoza shughuli za uchaguzi.
Ameyasema hayo leo 26,Oktoba 2025 wakati wa kuwaapisha wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura ambapo wasimamizi 2034 wa majimbo ya Kwimba na Sumve wamepata mafunzo katika vituo mbalimbali
"Kafanyeni kazi kwa kuzingatia sheria, tumieni nyaraka hizi tulizowapa kusoma na kuelewa ili mkajiepushe kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa, kwa wananchi na kwa mawakala"
Amewasisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha uchaguzi katika vituo vyote, pia amesisitiza umakini na lugha nzuri zenye staha zitumike kujibu watu watakaokuwa na maswali ya uelewa.
Katika mafunzo hayo ameshiriki Msimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo ya Kwimba na Sumve Bi. Jane Mallongo ambaye amewataka wote waliopata mafunzo kwenda kuzingatia yale waliyofundishwa ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa usahihi.
Naye Afisa Uchaguzi Bi. Grace Ishengoma amesisitiza wasimamizi wote kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwa wakati ili itakapotimu saa moja asubuhi ya tarehe 29,Oktoba 2025 zoezi la kupiga kura lianze.
Wasimamizi walioshiriki mafunzo hayo wameahidi kwenda kufanya kazi kulingana na taratibu walizoelekezwa
" mafunzo haya yatatusaidia kufanya kazi vizuri,nitumie wasaa huu kuwahamasisha wananchi wote waliojiandikisha wafike kwenye vituo vya kupigia kura tutawahudumia vizuri" amesema Mwalimu Maduka


Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.