WATAALAMU WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO
Posted on: July 22nd, 2025
Kamati ya maandalizi ya Mwenge ya Mkoa wa Mwanza imewataka wasimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo Wilayani Kwimba kuongeza kasi ili ya utekelezaji wa miradi ili kukamilisha miradi kwa wakati.
Wameyasema hayo leo 22,Julai 2025 wakati wakifanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi itakayopitiwa na mwenge wa Uhuru 2025
" ongezeni juhudi katika usimamizi, wahandisi na wasimamizi wengine jitahidini kufanyia kazi maelekezo na ushauri unaotolewa na viongozi wanaopita kukagua miradi hii ili iweze kukamilika kwa wakati" amesema James Mratibu wa Mwenge Mkoa
Naye katibu Tawala Wilaya ya Kwimba Ndugu Mohamed Ngasinda amewataka wataalamu wote kwenda kufanyia kazi maelekezo na ushauri uliotolewa ili utekelezaji wa miradi ukamilike kwa wakati.
Aidha Ngasinda amewataka wasimamizi wote wa shughuli za maandalizi na mapokezi ya Mwenge kufanya kazi kwa weledi huku akisisitiza hamasa itolewe kwa wananchi ili ifikapo 28, Agosti 2025 Wananchi wote washiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao utapokelewa katika kijiji cha Maligisu ukitokea Wilayani Magu.
Wataalamu walioshiriki ziara hiyo wameahidi kwenda kutekeleza maelekezo yaliyotolewa ili kuhakikisha shughuli zote zinatekelezwa na kukamilika kama ilivyokusudiwa.