Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka watendaji wa Kata kuwahamasisha wananchi kuzingatia ulaji bora wa vyakula vyenye lishe hasa wanawake wajawazito na watoto.
Ameyasema hayo kwenye kikao cha tathmini ya lishe kilichofanyika leo 23 Oktoba 2024 ambapo tathmini imeonyesha kuwa baadhi ya kata bado ina watoto wenye utapiamlo
" watendaji nendeni mkawahamasishe wananchi kula chakula kinachozingatia makundi yote ya vyakula, waelekezi wananchi kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo yao" Ludigija
Aidha Mkuu huyo amesisitiza wanawake wajawazito washauriwe kuhudhulia kliniki na wasisitizwe kuzingatia maelekezo yote wanayopewa kliniki ikiwa ni pamoja na kumeza dawa za kuongeza damu ili kuepuka kupata watoto wenye magonjwa mbalimbali kama kichwa kikubwa, mdomo wazi na magonjwa mengine.
Akiwasilisha taarifa ya lishe ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 Ema Kalolo Afisa Lishe amesema Shule zote zinatoa chakula kwa wanafunzi japo siyo wanafunzi wote wanaopata chakula kwani wengine wazazi wao hawajachangia vyakula kwaajili ya watoto wao
" niwaombe watendaji, walimu na maafisa Elimu Kata muendelee kuwahamasisha wananchi kuchangia vyakula kwaajili ya watoto shuleni, maana watoto ambao hawapati chakula wanapata wakati mgumu kushinda na njaa shuleni"
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt.Amon Mkoga ametumia wasaa huo kuhamasisha elimu iendelee kutolewa ya lishe kwa wananchi hasa wajawazito, pia amewataka watendaji kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.