WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO
Posted on: February 27th, 2025
Waheshimiwa madiwani wawataka watendaji wa Kata ya Ng'undi na Nyamilama kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Wameyasema hayo leo Februari 27,2025 kwenye mkutano wa baraza la madiwani siku ya kwanza ambapo taarifa za maendeleo ya kata zimewasilishwa huku kata hizo mbili zikionekana kulegalega katika ukusanyaji mapato ukilinganisha na kata nyingine.
Aidha wametumia mkutano huo kuwataka watumishi wasioishi maeneo yao ya kazi kuhamia katika maeneo yao ya kazi ili kutekeleza majukumu yao kwa wakati na kuhakikisha wananchi wanapata huduma muda wote wanapohitaji kuhudumiwa.
Katika mkutano huo taarifa za taasisi mbalimbali zimewasilishwa, na taasisi ya TARURA imetakiwa kuongeza usimamizi kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara ili miradi ikamilike kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.