Mkuu wa Idara ya Utawala Bi. Jane Mallongo amewataka watumishi kuzingatia taratibu,sheria na kanuni za utumishi wa umma huku akiwasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Ameyasema hayo leo 24 Novemba 2025 wakati wa kikao kazi na mafunzo kwa watumishi walioajiriwa hivi karibuni wa Idara ya utawala ambao ni watendaji wa vijiji na Kata
" watendaji wa Kata na Vijiji nyie ni viongozi katika maeneo mlikopangiwa kufanya kazi, nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa weledi, zingatieni kanuni za utumishi wa umma, wahudumieni wananchi kwa upendo na hakikisheni mnatimiza wajibu wenu" amesema Malongo
Bi Jane amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano kati yao na watumishi wengine na wananchi wataokwenda kuwahudumia huku akisisitiza kujifunza tamaduni za wananchi wa Kwimba ili waweze kuishi vizuri katika maeneo yao ya kazi.
Aidha amewataka kuzingatia nidhamu na maadili ambapo amewataka kufika kazini kwa wakati, mavazi yenye haiba ya utumishi wa umma na kuhakikisha wanakwenda kuwa chachu ya maendeleo kwa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Katika mafunzo hayo ameshiriki Bi. Khadija Mkelenga Afisa Utumishi ambaye amewataka watumishi hao kujiamini wanapotekeleza majukumu yao, pia amewasisitiza kutoa taarifa kwa viongozi wao wanapopata changamoto katika kazi.
Watumishi hao wameishukuru Serikali kwa kupata ajira, pia wameushukuru uongozi kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mafunzo na wameahidi kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu walizoelekezwa.

Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.