WATUMISHI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI WAHAMIA JENGO JIPYA LA UTAWALA
Posted on: June 30th, 2025
Hayawihayawi sasa yamekuwa, ilikuwa ni shauku ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupata ofisi nzuri na zenye ubora.
Shauku yao imetimia lei Juni 30,2025 baada ya watumishi hao kuhamia rasmi kwenye jengo la utawala la Halmashauri hiyo ambalo limejengwa katika Kata ya Ngudu Kijiji cha Icheja
"binafsi nina furaha kubwa kuhamia hapa kwenye hizi ofisi maana ofisi zetu zilikuwa zimechoka sana, lakini hapa kuna hadhi nzuri tunajisika kweli tuko ofisini"
amesema Mkuu wa kitengo cha Mazingira Deogratias Makungu
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Amon Mkoga amewataka watumishi kutumia ofisi hizo vizuri na kutunza miundombinu ya ofisi hizo ili jengo lisiwahi kuchakaa.
Pia amewataka watumishi wote kufika ofisini kwa wakati na kutekeleza majukumu yao ipasavyo bila kutengeneza visingizio.
Aidha Mkurugenzi Mkoga ametumia wasaa huo kuutarifu umma kuwa kuanzia leo juni 30,2025 huduma zote za Halmashauri zitapatikana katika jengo jipya la Utawala hivyo wananchi wote wanakaribishwa kupata huduma zote.
Kukamilika kwa jengo hili kutarahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi, kwani hawatapata taabu ya kuwatafuta wataalamu maeneo tofauti kama ilivyokuwa hapo awali ambapo ofisi zilikuwa maeneo tofauti kwamfano ofisi ya kilimo na ujenzi
" hapa huduma zitapatika kwa wepesi kwanza hakuna ule usumbufu wa wataalamu kakaa maeneo tofauti hapa watumishi wote tupo eneo moja, hili ni jambo zuri" amesema Afisa Utumishi Patrick Lubasha