Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Ngwilabuzu Ludigija amewataka wauguzi kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa
"niwapongeze sana kwa shughuli ambazo mmezifanya za utoaji wa huduma kwa wananchi,pia mmefanya usafi wa mazingira hongereni sana" ameyasema hayo leo Mei12,2025 kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani, ambayo yameadhimishwa katika hospitali ya Wilaya ya Kwimba.
Mkuu huyo amewasihi kuendelea kufanya kazi bila kuzingatia changamoto wanazokumbana nazo katika kazi hiyo,pia amewasisitiza kwenda kuishi kiapo walichoapa cha kutoa huduma bora
Aidha amewapongeza kwa kutoa zawadi kwa wagonjwa walioko wodini ambapo vitu mbalimbali vimetolewa ikiwa ni pamoja na sabuni za kufanyia usafi
" niwapongeze kwa kazi nzuri, pamoja na changamoto ambazo mmeeleza hapa lakini bado mnatoa huduma vizuri,nazani kwa mara ya kwanza niwapongeze mimi naamini katika kutenda mema na kuwatendea wengine mema, nimekuwa nikija marakwamara Nimefurahia kuona Muuguzi wa chumba cha watoto wachanga mahututi (HDU) kuna huduma nzuri, wauguzi wale wanahitaji pongezi sana
Mimi pia nimzazi sipendI kusikia vifo vya mama na mtoto na tunaendelea kuwahimiza wajawazito kuwahi hospitali tukitegemea huku wanakuja kupata huduma bora, natamani kiapo mlichokila na maneno yaliyomo humu mkayaishi ili tuibadirishe Wilaya hii"
Pia amewataka kuambizana ukweli bila kuoneana haya pale ambapo muuguzi mmojawapo anatoa huduma mbovu kwa wagonjwa na kusababisha kuharibu sifa ya wauguzi wote.
Aidha amewataka wauguzi kuwahi kazini kulingana na ratiba zao, pia amewasisitiza kuzingatia taratibu za kukabidhiana wagonjwa ili kuwe na utaratibu mzuri wa matibabu.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Fredrick Mgarula amewataka kuendelea kuboresha huduma bila kujali changamoto"nawaasa sana tujitahidi kutoa huduma vizuri"
Katika maadhimisho hayo ameshiriki Kaim Mkurugenzi Mwlm. Emmanuel Katemi ambaye amewapongeza wauguzi kwa kuipenda kazi yao na amewataka kwenda kutumikia vizuri kiapo walichoapa mbele ya mgeni rasmi, kiapo kinachohimiza uwajibikaji,
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.