• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

WAZAZI WAASWA KUSIMAMIA USALAMA WA WANAFUNZI

Posted on: October 7th, 2023


Mkurugenzi wa Sera na mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndugu. John Mihayo Cheyo amewaasa wazazi wa wanafunzi kuhakikisha wanaimarisha usalama wa wanafunzi, huku wakihakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayeacha masomo kwa sabanu ya utoro,mimba, kuoa au kuolewa na mambo mengine.


Ameyasema hayo jana Oktoba 7,2023 kwenye mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari Bupamwa ambapo alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hiyo


"wazazi saidieni watoto wasiache Shule, pendeni kuona mafanikio ya watoto wenu wakimaliza Shule na kufaulu,zuieni utoro, narudia tena wanafunzi wasilale nyumbani wakawa watoro shuleni na wasiolewe " amesema Cheyo


Shule hiyo imeonekana kuwa na changamoto ya utoro na baadhi ya wanafunzi kuacha Shule kwani wanafunzi waliohitimu ni 93 kati ya 153, wengi wameonekana kuacha Shule kwa sababu ya umbali kutoka nyumbani kwao hadi shuleni na sababu nyingine


" tumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ameiona changamoto waliyokuwa wanaipata wanafunzi wanaotokea vijiji vya Itegamatu, Kiliwi na Dodoma sasa ameleta fedha, Shule mpya inajengwa Kiliwi nadhani hatutasikia tena wanafunzi watoro au kuacha Shule" Cheyo


Katika mahafali hiyo mgeni rasmi ametatua changamoto za Shule hiyo ikiwa ni pamoja na kununua tangi la maji la thamani ya milioni 1.5 ili kuhakikisha upatikanaji wa Maji shuleni, vilevile changamoto nyingine zikiwemo za miundombinu ya mabweni ameahidi kwenda kufuatilia wizarani Ili miundombinu hiyo ikamilishwe.


Mkurugenzi huyo amewahamasisha Walimu na watumishi wengine wa Shule hiyo kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ufaulu wa Shule hiyo "leo nimekuja na zawadi za wanafunzi waliofanya vizuri,  Walimu na wapishi, niwaombe muendelee kufundisha vizuri na kuwasaidia wanafunzi wote wafaulu,nawapongeza sana kwa kufuta ziro matokea ya kidato cha nne  mwaka jana muendelee hivyo msirudi nyuma" Cheyo


Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Herman Shingisha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya kiongozi shupavu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za ujenzi wa madarasa na hivyo kuondoa kero ya uhaba wa madarasa  na Shule mpya.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.