Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa( MB) leo 18,Mei 2025 ameweka jiwe la Msingi kwenye jengo la Utawala la Halmashauri ambapo amewaelekeza wasimamizi wa jengo hilo kukamilisha jengo kwa wakati ili Wakuu wa Idara na Vitengo wahamie katika ofisi hizo
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu amezindua mradi wa maji Hungumalwa na amekagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha michezo ) Sport Academy) kisha akaongea na Wananchi katika viwanja vya Kwideko Ngudu ambapo ametoa taarifa na maelekezo mbalimbali.
"nimekuja kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza miradi yote ya maendeleo, sasa niwakati wa kuwambia wananchi nini kimefanyika na kinachoendelea kufanyika
Aidha amewataka Wabunge kuendelea kutoa taarifa za mapendekezo ya miradi ambayo bado inahitaji kutekelezwa hapa Kwimba, "nitoe wito kwa waheshimiwa Wabunge kuendelea kutuambia maeneo yanayohita msisitizo au usaidizi wetu kwamfano kwenye eneo la Elimu Msingi na Sekondari na hakikisheni watoto wanaenda Shule.
Mheshimiwa Majaliwa amewataka wazazi kupeleka watoto wao vyuo vya VETA, Malya FDC na Malya Chuo cha michezo ili wapate ujuzi ambao utawasaidia kupata utaalamu mbalimbali ukiwemo utalaam wa michezo.
Pia amewataka Wakurugenzi na Maafisa Elimu kusimamia ufundishaji ili kuongeza ufaulu, pia amesisitiza ikama za walimu shuleni zizingatiwe.
Aidha Waziri Mkuu amewataka Wahandisi wanaosimamia miradi ya maji kuhakikisha wanaongeza juhudi katika kusimamia miradi hiyo ili ikamilika kwa wakati ili wananchi wa Ngudu wapate maji ya kutosha.
Katika ziara hiyo ameshiriki Mhe. Mansour Shanif Mbunge Jimbo la Kwimba ambaye ameeleza jinsi Serikali ya awamu ya sita inavyotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Elimu,Afya,umeme,barabsra na maji.Pia amemuomba Waziri Mkuu kusaidia mradi wa maji Ngudu kukamilika mapema ili kero ya ukosefu wa maji iishe.
Naye Mbunge wa Jimbo la Sumve amemshukuru Waziri Mkuu kwa kuon
" kwa kitendo hiki cha heshima ulichokifanya cha kuja kwimba kimeimarisha Chama Cha Mapinduzi, naomba kamwambie Mheshimiwa Rais kuwa tumejipanga kumpa kura za kishindo"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.