• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Waziri wa Nishati na Madini Azindua Mradi Kabambe wa Umeme Vijijini REA Awamu ya Tatu Wilayani Kwimba

Posted on: July 14th, 2017


Naibu waziri wa Nishati na Madini  DKT. Medard M.Kalemani amezindua Mradi kabambe wa Umeme Vijijini REA awamu ya tatu Mkoani Mwanza tarehe 13 Julai 2017. Uzinduzi huo Kimkoa Umefanyika katika kijiji cha Nyamatala kata ya Ngulla Wilayani Kwimba.

Tumelenga kuwaunganishia wateja 720,515 katika mkoa wa Mwanza tunaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza waanze kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuongeza mnyororo wa thamani katika mazao. Hayo yamesemwa na Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos  Maganga wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyamatala.

Naye Naibu waziri wa Nishati na Madini  DKT. Medard M.Kalemani  amesema Mradi huu wa  umeme vijijini hauna Chama wala Dini na utawekwa kwenye kila nyumba hivyo basi vijiji  na vitongoji vyote vya Mkoa wa Mwanza vilivyoachwa na Mradi wa REA awamu ya pili  vitawekewa Umeme bila kusahau Taasisi za Umma  ambazo ni  Vituo vya Afya, Zahanati,Makanisa ,Misikiti,Shule pamoja na Mitambo ya Maji.




Naibu Waziri wa Nishati na Madini  DKT Medard M.Kalemani akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nyamatala Wilayani Kwimba wakati wa Uzinduzi wa Umeme Vijijini REA awamu ya tatu.

Mkoa wa Mwanza umeunganishwa na umeme Mkubwa wenye nguvu ya  400kb, Mhe Naibu Waziri DKT. Medard   amewaomba wananchi waanze kujenga viwanda vidogovidogo,viwanda vya kati na viwanda vikubwa kwa ajili ya kuleta maendeleo katika maeneo yao.

Mkoa wa Mwanza una jumla ya vijiji  mia tatu arobaini na tatu (343) ambavyo havijapata umeme hivyo basi  vijiji 174 vya Mkoa wa Mwanza vinakwenda kupata umeme ndani ya miezi ishirini na nne (24) kuanzia sasa na vitakamilika mwezi Aprili 2019 na vijiji   mia moja sitini na tisa (169) vilivyobaki vitapata umeme kuanzia mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2020/2021. Mhe. Naibu Waziri DKT. Medard  ameyasema hayo wakati wa kumtambulisha na kumkabidhi Mkandarasi NIPO GROUP Kampuni ya kizalendo ya kitanzania ambayo itafanya kazi ya uwekaji wa umeme Vijijini REA awamu ya tatu.

Aidha ametoa maelekezo mbalimbali  kwa kampuni ya kizalendo  NIPO GROUP kuhakikisha inaajiri wakandarasi katika maeneo watakayokuwa wanafanya kazi.

“Kwimba,Sumve Ngudu na maeneo mengine tunataka wakandarasi wazalendo wa maeneo hayo wapate ajira”




Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mwanza Bibi Sarah Assey(kulia) akiwa  na Kampuni ya kizalendo NIPO GROUP

Amemuagiza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mwanza Bibi Sarah Assey kuhakikisha anafungua ofisi ndogo za umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza.

“Meneja wa TANESCO fungua ofisi ndogo ya Umeme Nyamatara,Hungumalwa, Sumve na maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu weka muhudumu wa TANESCO Kwa ajili ya kuhudumia wateja”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela ametoa maelekezo kwa wakuu wa Wilaya wote na Wakurugenzi wa halmashauri wote kuwa kila mwezi apate taarifa Mkoani ya utekelezaji wa Mradi wa REA  awamu ya tatu.Pia amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya.

“Hakuna mtanzania mwenye akili timamu  wala asiye mtanzania  asiyeona kazi anazozifanya  tunamuombea sana Mwenyezi Mungu amzidishie ampe afya ya mwili na akili ili aweze kutupeleka kwenye nchi ya Maziwa na Asali”


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongera Akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Umeme Vijijini awamu ya tatu.





Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.