Kamati ya mikopo ngazi ya Kata wapata mafunzo ya namna ya kusajili vikundi vya mikopo, mafunzo yametolewa na Maafisa maendeleo ya jamii wakiongozwa na Mkuu wa Idara hiyo Bi. Rozalia Magoti. Kamati hizo zimefundishwa kanuni na miongozo inayotumika kutoa mikopo kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Mafunzo hayo yamefanyika jana Oktoba 22,2024 kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu ambapo Watendaji wa Kata, wataalamu ngazi ya Kata na Polisi Kata wameshiriki mafunzo hayo.
Kikubwa zaidi katika kanuni hizo umri wa vijana umeongezwa ambapo awali vijana waliokuwa wanakopa mikopo waliishia umri wa miaka 35 lakini kwa sasa vijana wanaishia umri wa miaka 45.
Kamati hizo zimetakiwa kwenda kuwahamasisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujitokeza kuchukua mikopo ambapo zaidi ya milioni 700 imetengwa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Dirisha la mikopo limefunguliwa ambapo elimu imeanza kutolewa kwa viongozi na wananchi ili waone umuhimu wa kuchukua mikopo hiyo kwaajili ya kufanya ujasiliamari utakaosaidia kuinua uchumi wao.
Bi . Magoti amesisitiza kuwa utoaji wa mikopo kwa sasa umerahisishwa zaidi kwani mikopo itatolewa kwa kikundi japo ndani ya kikundi kila mtu anaweza kuwa na shughuli tofauti " siyo lazima wanakikundi mfanye biashara moja kila mtu anaruhusiwa kuwa na biashara yake lakini mkopo mtapewa kama kikundi"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.