ZAIDI YA MITI 900 YAPANDWA KATIKA KAMPENI YA "MTI WA MAMA"
Posted on: January 27th, 2025
Katika kuadhimishla siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Kwimba imeazimisha siku hii kwa kupanda miti katika Shule ya Sekondari mpya ya Dr. Samia Kata ya Malya.
Ikiwa ni mikakati ya kutunza mazingira na kuungana na Serikali katika kuboresha mazingira kwa kutunza miti siku ya leo Januari 27 imepambwa na " mti wa mama" ambapo miti zaidi ya 900 ikiwa ni miti ya matunda na mbao.
" kampeni ya Mti wa Mama itakuwa endelevu" haya yamesemwa na mtendaji wa Kijiji cha Malya wakati akiwasilisha taarifa ya upandaji miti.
Akiwasilisha taarifa hiyo amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuleta fedha zaidi ya milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Malya shule ambayo imepewa jina la Dr. Samia, shule hiyo imeanza rasmi mwaka huu ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza wameshaanza masomo.
Mgeni rasmi wa tukio hilo Ndugu Mohamed Ngasinda Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba kwa niaba ya Mkuu ya Mkuu wa Wilaya amewataka wanachi wote kuendelea kupanda miti ili kutunza mazingira
" ndugu wananchi lengo la kukutana hapa ni kupanda miti aina mbalimbali ikiwa nipamoja na miti ya matunda na miti ya mbao ili kuunga mkono juhudi za Rais za utunzaji wa mazingira" Ngasinda
Amesisitiza wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti na kutumia nishati safi ya kupikia hii itasaidia kuondokana na ukataji wa miti
Mwenyeki wa Halmashauri wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Thereza Lusangija ametumia wasaa huo kuwahamasisha wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wanakwenda Shule bila utoro maana shule imejengwa karibu na makazi yao.
Aidha Mwenyiki wa CCM Wilaya ya Kwimba Mhe. Sabana Lushu amewapongeza viongozi wote waliosimamia ujenzi wa Shule pia amewapongeza kwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt.Amon Mkoga amewataka wasimamizi wa Shule zote kuendeleza utaratibu wa kupanda miti pia amemtaka Mkuu wa Shule hiyo ya Dr. Samia kuhakikisha shule inakuwa matokeo mazuri" Mkoga