Miundo mbinu ya ghala na soko inayotekelezwa na Mradi wa MIVARF katika kijiji cha
Mahiga kata ya Mwang'halanga.
UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ni miongoni mwa Wilaya tatu za Mkoa wa Mwanza zinazotekeleza Program ya Miundo mbinu ya masoko, uongezaji thamani ya mazao na uboreshaji wa huduma za kifedha vijijini (MIVARF). Mradi huu ulianza kutekelezwa Kwimba mnamo Machi 2013 kwa kuanza na vikao vya wadau (Hamasa).
ENEO LA MRADI
Kijiji cha Mahiga ndilo eneo la kitovu cha Mradi wa MIVARF, kina idadi ya watu 3,202.Kijiji hiki kipo kata ya Mwang’halanga yenye wakazi 11,099. Kijiji hiki kipo umbali wa kilomita 8 kutoka Makao Makuu ya Wilaya (Ngudu Mjini)
Program ya miundombinu ya masoko, uongezaji thamani ya mazao na uboreshaji wa huduma za kifedha vijijini (MIVARF) ililenga kuwekeza katika maeneo ambayo tayari Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekwisha wekeza kiasi kikubwa cha fedha lakini haijakamilisha mnyororo wa thamani wa mazao husika. Eneo lililopendekezwa kwa Wilaya ya Kwimba ni kijiji cha Mahiga ambapo tayari kulikuwa na bwawa kwa ajili ya umwagiliaji wa zao la mpunga.
Mnyororo wa thamani unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupitia program ya MIVARF ni mnyororo wa thamani wa zao la MPUNGA, ambapo mkulima anafundishwa kanuni mbalimbali za kilimo bora kupitia Mtoa Huduma aliyeingia Mkataba na MIVARF kampuni ya LITENGA kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakulima pamoja na kuwaunganisha na masoko.
Kutokana na kuwa Halmashauri iliwekeza katika Skimu ya Umwagiliaji katika kijiji cha Mahiga na kwamba bado mnyororo wa thamani haukuwa umekamilika, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilipendekeza Mradi huo kuwa katika eneo linalozunguka Skimu ya Umwagiliaji Mahiga kwa kujumuisha kata za Mwang’alanga, Nyamilama na Lyoma.
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA PROGRAM KUFIKIA JANUARI 31, 2017
Ujenzi na ukarabati wa miundombinu.
Ukarabati wa barabara ulifanyika kuunganisha maeneo ya Mradi na kitovu cha Mradi ambacho kipo kijiji cha Mahiga. Mradi huu unajumuisha kata tatu za Mwang’halanga (eneo kuu la Mradi - Mahiga), Nyamilama na Lyoma.
Ukarabati wa barabara za jumla ya kilomita 14.2 ulifanyika kwa kiwango kinachokubalika. Barabara zifuatazo zilikarabatiwa kwa jumla ya Tshs. 722,971,170.00; Ngudulugulu-Mwang’halanga - Nkungulu (11.1km), Mahiga-Luhala (1.6km) na Mahiga - Bwawa la umwagiliaji (1.5km).
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea na ujenzi wa miundo mbinu ya ghala na soko yenye thamani ya Tshs. 617,423,800.00. Thamani hiyo inajumuisha vipengele 5 vya ujenzi wa ghala, soko, tenki la kuvunia maji ya mvua, nyumba ya mlinzi, choo na mitaro ya kudhibiti maji ya mvua. Mradi huu ni muhimu kwa ajili ya wakulima kuweza kuhifadhi mazao yao baada ya kuvuna, kuendesha mfumo wa stakabadhi ghalani pamoja na kutumia miundombinu ya soko kwa ajili ya shughuli za biashara mbalimbali kijijini hapo.
Ununuzi wa Vifaa vya Ghala
Halmashauri imesimamia ununuzi wa vifaa vya ghala ambavyo ni kipima unyevu (Moisture meter), Mzani (weighing scale), turubai 2 na vifaa vya zima moto 6 (Fire extinguishers). Vifaa hivi vilinunuliwa na kampuni ya M/S Mambwe Trading ya S.L.P 10027, ARUSHA kwa thamani ya Tshs. 23,820,000.00, vifaa hivi vilipokelewa 18/12/2016 na tarehe 18/01/2017 vifaa hivyo vilikaguliwa na wataalam kutoka ofisi za Wakala wa Vipimo Mwanza na Ofisi ya Zima moto na Uokoaji (Mwanza) wakishirikiana na mtaalam kutoka ofisi ya Idara ya Kilimo (Kwimba). Taarifa ya mapokezi ya vifaa na ukaguzi wake zilitumwa MIVARF Makao Makuu kwa ajili ya kukamilisha taratibu za malipo.
Vifaa vilivyotolewa na Program ya MIVARF
Katika kuhakikisha Program ya MIVARF inatekelezwa kwa ufanisi Wilayani Kwimba, Program ilinunua vifaa vifuatavyo kwa ajili ya kuhakikisha wataalam wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi:
Kompyuta: Kwa ajili ya kurahisisha utoaji taarifa
Scanner: Kwa ajili ya kuhakikisha taarifa zinatumwa kwa wakati
Pikipiki: Program imetoa pikipiki mbili aina ya YAMAHA kwa ajili ya kumwezesha Mhandisi wa Ujenzi pamoja na Mratibu wa Program wanaweza kufika maeneo mbalimbali ya Program.
Hali halisi ya ujenzi hadi kufikia tarehe 13/03/2017
Na
|
Kipengele cha mradi
|
Hali halisi (Status)
|
Kazi ambazo zinaendelea kutekelezwa na ambazo bado hazijafanyika
|
1
|
Ghala
|
Ujenzi umekamilika
|
Maelekezo madogo madogo ya kufanyiwa kazi na yanaendelea:
|
2
|
Soko
|
Ujenzi umekamilika
|
Kufunga gata za kuvunia maji ya mvua
|
3
|
Choo
|
Jengo limekamilika
|
Uwekaji wa maungio ya mfumo wa maji safi na taka unaendelea.
|
4
|
Mitaro ya kudhibiti maji ya mvua
|
Uchimbaji na ujenzi umekamilika
|
Hakuna
|
5
|
Tenki la maji
|
Ujenzi umekamilika
|
Bado maunganisho ya mfumo wa maji safi
|
6
|
Kibanda cha mlinzi
|
Jengo limekwisha kamilika kwa ajili ya matumizi.
|
Marekebisho madogo madogo aliyoelekezwa Mkandarasi ikiwemo upakaji varnish frame za madirisha.
|
Miradi ya ujenzi wa miundo mbinu: Muda wa kuanza na kukamilika
Na. |
Mradi |
Kuanza |
Kukamilika |
Gharama ya Mradi (Tshs) |
Mchango wa Halmashauri (5%) |
Maelezo |
1.
|
Ukarabati wa barabara ya: Ngudulugulu-Mwang'halanga-Nkungulu (11.1km), Mahiga-Luhala (1.6km) na Mahiga-Bwawa la Umwagiliaji (1.5km)
Mkandarasi: Mumangi Construction Ltd |
02/10/2013
|
17/03/2014
|
722,971,170
|
6,000,000
|
Mradi umekamilika
|
2.
|
Mradi wa ujenzi wa ghala na soko –Mahiga.
Mkandarasi: Glinda Builders Ltd |
24/02/2015 (Baada ya kuwasilisha dhamana ya utendaji kazi
|
07/05/2016
|
617,423,800 |
-
|
Mradi umekamilika, marekebisho madogo madogo yanaendelea.
|
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.