Kilimo cha Pamba Kinavyotekelezwa Wilayani Kwimba
1.0: HISTORIA YA KILIMO CHA ZAO LA PAMBA WILAYANI KWIMBA
Pamba ni zao kuu la biashara katika wilaya ya Kwimba zaidi ya asilimia 70 ya wakulima walikuwa wanajishughulisha na kilimo cha pamba. Kwa kipindi cha miaka mitatu zao la pamba limekuwa likishuka uzalishaji kama ifuatavyo; mwaka 2014/2015 uzalishaji ulikuwa kilo 7,596,916, 2015/2016, kilo 4,512,420 na 2016/2017 kilo 2,051,122.
Katika vipindi vyote hivi vitatu kulikuwepo na mafanikio na changamoto mbalimbali zilizojitokeza. Mafanikio machache yaliyopatika kupitia kilimo cha pamba kwa mkataba ni upatikanaji wa pembejeo kwa mkopo, uwezeshwaji wa huduma za ugani kutoka kwa makampuni na uundaji wa Vikundi vya wakulima (FBGs). Mbali na mafanikio machache kulikuwa na changamoto zilizokwamisha kilimo cha mkataba zikiwemo; ukopeshwaji usio fuata taratibu, urejeshwaji mdogo wa madeni, pembejeo zisizo na ubora, makampuni kushindwa kutimiza masharti ya mkataba, bei ya dogo ukilinganisha na gharama za uzalishaji na mvua zenye mtawanyiko usioridhisha.
2.0: UTEKELEZAJI WA KILIMO CHA PAMBA KWA MKATABA MSIMU 2016/17
Katika msimu wa kilimo cha pamba 2016/17, Wilaya ya Kwimba imeitikia wito wa Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufufua zao la pamba ambalo kwa takribani miaka mitano uzalishaji wake umeshuka. Lengo ni kuwezesha uzalishaji mkubwa wa pamba kama malighafi wenye tija ili kuwezesha uendeshaji wa viwanda.Kwa kutambua kuwa zao hili lina mnyororo mrefu wa thamani.
Katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John .V.K.Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha zao la pamba linafufuliwa kwa kuongeza tija na uzalishaji. Wilaya ya Kwimba iliandaa andiko lenye vigezo na masharti ya kuwekeza katika kilimo cha pamba na kulituma kwa Makampuni 13 ambayo ni Afrisian Ginning, SM Holdings, ICK Cotton, Kahama Oil Mills, Kahama Cotton Company, Alliance Ginneries, Birchad Oil Mills, Olam (T), Aham Investment Co. Ltd, Fresho Investment, Gaki Investment Co. Ltd na Nida Textile Mill. Makampuni hayo yalitumiwa mwaliko wa kuomba kuwekeza katika kilimo cha pamba kwa mkataba kuanzia msimu 2016/2017. Kati ya makampuni 13 ni makampuni matatu (3) ambayo ni SM Holdings, Afrisian Ginning na ICK Cotton ziliomba kuwekeza na baadaye Halmashauri ilifunga mkataba na kampuni hizo kwa kipindi cha miaka mitatu.
3.0: MIKAKATI ILIYOTUMIKA KUFANIKISHA KILIMO CHA MKATABA
Timu za uhamasishaji wa ngazi ya Wilaya kupita kila kijiji kuelemisha na kuamsha ari ya kufufua kilimo cha pamba walau kila kaya kulima ekari moja.
Ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika shughuli za kilimo cha pamba hususan Bodi ya Pamba, TGT na wataalam kutoka kampuni Quton.
Kugawa maeneo ya uwekezaji kwa kuzingatia mahitaji ya Kampuni; SM Holdings tarafa ya Ibindo, Afrisian Ginning tarafa ya Mwamashimba na ICK Cotton tarafa ya Nyamilama, Ngudu na Ngulla. Lengo la Wilaya kugawa uwekezaji kwa maeneo ni kuondoa muingiliano na utegeaji katika uwekezaji.
Uundwaji wa Vikosi Kazi ngazi ya Wilaya na Vijiji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa kilimo cha pamba.
Kuboresha huduma za ugani kwa kuwapa maafisa ugani pikipiki, mafuta na posho kwa ajili ya kusimamia majukumu yao.
Kuanzisha shamba darasa la viongozi wa kamati ya Ulinzi na Usalama na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ili kuhamasisha jamii kutekeleza kilimo cha Pamba.
Kuanzisha mashamba darasa katika shule za msingi na Sekondari ili kufufua elimu ya kujitegemea shuleni na kuandaa wakulima wa baadaye.
Usimamizi thabiti wa utekelezaji wa majukumu yaliyoanishwa kwenye mkataba.
4.0: HALI YA USAMBAZAJI PEMBEJEO
Kwa msimu 2016/17, Wilaya ilipata mgawo wa mbegu tani 500 UK 91(manyoya) kutoka Bodi ya pamba. Kutokana na mahitaji kuongezeka hadi kumalizika kwa msimu wa kupanda jumla ya tani 518 za UK 91 na tani 80 za UKM08 (kipara) zilisambazwa vijijini. Kati ya mbegu hizo jumla ya tani 488 za UK 91 na tani 78 za UKM08 zilichukuliwa na wakulima. Makisio ya ekari zilizotarajiwa kulimwa zilikuwa ni ekari 61,873.
Kutokana na changamoto ya hali ya hewa ilisababisha wakulima kulazimika kupanda zaidi ya mara moja na wengine kushindwa kabisa kupanda. Makisio yalishuka hadi kufikia ekari 46,000. Hata hivyo katika zoezi la uhakiki wa mashamba ambalo limekamilika mwezi Machi, jumla ya ekari 24,025 zimebainishwa kupandwa na kuota vizuri.
Kulingana na makisio ya ekari 61,873 ambazo zilitokana na usambazaji wa mbegu, mahitaji ya viuadudu yalikuwa chupa 165,000. Hadi kufikia sasa ni chupa 59,040 ambazo zimesambazwa vijijini, kati ya viuadudu hivyo chupa 46,840 zimetolewa na makampuni, chupa 11,500 zimetolewa na CDTF na chupa 700 zimetolewa na Bodi ya Pamba. Kwa upande wa vinyunyizi jumla ya vinyunyizi 189 vimesambazwa na vinyunyizi 148 vimechukuliwa na wakulima.
4.1: Ukopeshwaji wa pembejeo kwa kila kampuni
KAMPUNI
|
MBEGU
|
DENI LA MBEGU (TShs)
|
VIUADUDU (CHUPA)
|
DENI LA VIUADUDU
|
WAKULIMA WALIOKOPA MBEGU (Idadi)
|
|
UK 91
|
UK M08
|
|||||
SM HOLDINGS
|
91,387
|
47,856
|
173,760,500/=
|
14,068
|
28,136,000/=
|
5,472
|
I.C.K COTTON
|
227,237
|
0
|
167,070,128/=
|
22,803
|
45,606,000/=
|
5,493
|
AFRISIAN GINNING
|
123,650
|
30,178
|
104,415,500/=
|
10,034
|
20,068,000/=
|
3,193
|
JUMLA
|
442,276
|
77,396
|
444,618,128/=
|
46,905
|
93,810,000/=
|
14,158
|
Jumla ya Tsh 538,428,128.00 zimewekezwa na makampuni matatu zikiwa ni gharama ya mbegu na viuadudu.
5.0: UWEZESHWAJI WA SHUGHULI ZA KILIMO CHA PAMBA KWA MKATABA.
Katika kuendesha shughuli za kilimo cha pamba kwa mkataba, Halmashauri imechangia shilingi milioni 7.3 ambazo zilitumika katika zoezi la uhamasishaji wa kilimo cha pamba kwa kununua mafuta ya dizeli na petroli. Wilaya ilipokea pikipiki 10 na shilingi milioni 12 kutoka kwa makampuni, Shirika lisilokuwa la kiserikali la Gatsby Africa liliwezesha shilingi milioni 8. Fedha hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha shughuli za kilimo cha pamba hususan katika mambo yafutayo;
6.0: MAFANIKIO KUPITIA KILIMO CHA PAMBA KWA MKATABA.
7.0: CHANGAMOTO
8.0: MIKAKATI
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.