Jukumu kuu la Idara hii ni kuhamasisha, kuboresha na kusimamia utoaji wa huduma za maendeleo ya kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
usambazaji wa uuzaji wa pembejeo na zana za kilimo kutoka maduka ya watu binafsi.
Usimamiaji wa matumizi ya pembejeo za kilimo katika Vijiji/Mitaa/Kata.
Kutoa elimu/ushauri wa matumizi ya mbolea na madawa, kilimo mseto, usindikaji wa mazao, hifadhi ya udongo na matumizi bora ya ardhi, kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji wa mazao mbalimbali ya nafaka, Choroko, Dengu, Mihogo, Mpunga, Mtama ,Viazi vitamu,Alizeti na Mahindi kwa kuzingatia kanuni bora kwa wakulima mmoja mmoja au vikundi.
Kufanya tathmini kuhusu hali ya chakula na lishe katika Halmashauri.
Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Miradi ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agriculture Development Projects – DADPs).
Kuhamasisha na kusimamia shughuli za kilimo cha zao la Pamba.
Kufanya maandalizi na kushiriki maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane.