Huduma Zinazotolewa
Halmashauri ya wilaya ya Kwimba inatoa huduma mbali mbali katika upande wa elimu kama ifuatavyo;-
1. kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusiana na elimu na miongozo mbalimbali inayohusiana na kuboresha elimu.
2. kusimamia elimu ya watu wazima
3. kutoa ushauri kwa wazazi wanaohitaji kuhamisha wanafunzi
4. kupitisha fomu za kuhamisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
5. kuratibu na kupitisha likizo za walimu wa shule za sekondari na Msingi
6. kusimamia taaluma katika shule za Msingi na Sekondari kulingana na sera ya elimu.
7.kuratibu zoezi la kutoa takwimu za shule za sekondari na Msingi kwa kufuata miongozo.
8.kutoa ushauri wa kuboresha miundombinu katika shule za sekondari na msingi
9.kusimamia masuala yote yanayohusiana na elimu na kutoa ushauri kwa wazazi wanaohitaji kuhusiana na elimu
10.kukusanya na kuunganisha Tange ya walimu wa sekondari na Msingi katika shule zote na kuwasilisha katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W).
11. kusimamia sera ya elimu Msingi Bila Malipo katika shule zote.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.