HALMASHAURI YA WILAYA YA KWIMBA
IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA
Mkuu wa Idara ya Utawala na utumishi
Jane Malongo
Mawasiliano Na.0786218526
UTANGULIZI
Idara ya Utawala na Utumishi ni Idara inayojumuisha rasilimali watu na vitu ngazi za Vijiji Kata, tarafa na makao makuu ya Halmashauri. Hadi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ina jumla ya vijiji 119 na Kata 30 na tarafa 5.
UTUMISHI;
Ofisi ya Utumishi Ina jumla ya Maafisa Utumishi 6 na Kaimu Mkuu wa Idara 1. Idara hii ina majukumu mbalimbali yaliyogawanywa kwa maafisa utumishi waliopo ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Kushughulikia maslahi ya watumishi kama malalamiko, kusimamia mafunzo kwa watumishi, likizo, kusimamia utendaji kazi wa watumishi kwa kusimamia kanuni, sheria, nyaraka na taratibu za utumishi wa umma katika kuhudumia umma, kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao kama mshahara wa kila mwezi, makato, mikopo kwa watumishi pamoja na kusimamia ujazaji wa fomu za OPRAS.
MAJUKUMU YAMEGAWANYWA KAMA IFUATAVYO.
1. Kuratibu Mafunzo
Idara inawajibika kuratibu na kuandaa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kwa watumishi kulingana na mahitaji ya taasisi lakini pia kama haki ya mtumishi kuongeza elimu akiwa mahali pa kazi. Utaratibu wa kwenda kwenye mafunzo hayo uanzia katika Idara husika baada ya mtumishi kufanyiwa tathmini ya utendaji kazi wake pamoja na elimu aliyonayo, Idara upanga kumuweka mtumishi katika bajeti ili aweze kuhudhuria mafunzo au masomo kulingana na mahitaji na mapungufu aliyonayo. Utaratibu huu unatokana na matokeo ya kujaza fomu za Opras ambapo changamoto za utendaji kazi huonekana katika fomu hizo. Hata hivyo Maombi ya kuingia kwenye mpango wa mafunzo yanaanzia Januari hadi Machi ya kila mwaka.
2. Kuratibu Likizo
Idara inaratibu likizo zote za watumishi wa Halmashauri.
Watumishi wote wanatakiwa kujua kwamba likizo ni haki yao na ni muhimu kwao.Pia wanapaswa kujua kuwa utaratibu wa kwenda likizo uanzia kwenye Idara husika kwa Wakuu wa Idara kuandaa mzunguko wa likizo (Leave Roster) ya kila mtumishi kulingana na tarehe yake ya ajira .
3. Upimaji Utendaji kazi wa wazi (OPRAS)
Idara pia inaratibu zoezi la Upimaji Utendaji kazi wa wazi yaani OPRAS kwa watumishi. Opras ni muhimu kwa watumishi kwenda kozi kwani ni kigezo kimojawapo cha upandaji cheo, na pia inaonyesha mapungufu ya Mtumishi kwa hitaji la kwenda masomoni, inaleta ufananisi katika kutekeleza majukumu, inaleta ushirikiano n.k. Zoezi la Opras hufanyika kila mwanzo wa mwaka wa Serikali yaani Julai ambapo watumishi wote wanatakiwa kujaza malengo yao ya mwaka katika fomu hizo baada ya kukubaliana na wasimamizi wao wa kazi.
4. Mikopo ya Watumishi (1/3 ya Mshahara)
Watumishi wanatakiwa kujua kwamba unapokopa unatakiwa ubaki na I/3 ya mshahara wako na kwamba mikopo yote inaingizwa kupitia system ya LAWSON ili makato yaweze kukatwa kila mwezi.
5. Kushughulikia malimbikizo ya Watumishi
Watumishi wote wanatakiwa kujua kuhusu utaratibu mpya wa malimbikizo (arrears). Mtumishi yeyote aliepanda cheo na akachelewa kurekebishiwa mshahara akawa na madai ya malimbikizo au ajira mpya aliechelewa kupata mshahara akawa anadai malimbikizo haitaji kujaza fomu za malimbikizo (arrears) kwa sababu kwa sasa malimbikizo (arrears) yanalipwa moja kwa moja. Hivyo anachotakiwa kufanya ni kwenda kwa Afisa Utumishi anaeshughulika na malimbikizo (ARREARS) na kuona kama madai yako yatalipwa moja kwa moja au kuna shida yeyote.
6.Hali ya Utumishi na Utawala
Halmashauri ina jumla ya watumishi 3,247 kati ya mahitaji ya watumishi 4,751. Hivyo ina upungufu wa watumishi 1,504 kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Idadi ya watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
|
IDARA
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
MAPUNGUFU
|
|
UTAWALA
|
171 |
258 |
87 |
|
ELIMU MSINGI
|
2,416 |
1,659 |
757 |
|
ELIMU SEKONDARI
|
1,075 |
839 |
236 |
|
AFYA
|
1140 |
397 |
743 |
|
MAJI
|
34 |
28 |
6 |
|
UJENZI
|
29 |
20 |
9 |
|
KILIMO NA USHIRIKA
|
173 |
32 |
141 |
|
MIFUGO NA UVUVI
|
77 |
43 |
34 |
|
JUMLA
|
5115 |
3276 |
2013 |
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.