1.0: Utangulizi
Wilaya ya Kwimba ni moja wapo ya Wilaya kongwe kati ya Wilaya nane za Mkoa wa Mwanza. Katika kuhakikisha kuwa huduma muhimu zikiwemo za utawala zinasogezwa karibu na wananchi, mwaka 1973 Serikali iliigawa Wilaya ya Kwimba na kuanzisha Wilaya mbili za Kwimba na Magu. Pia mwaka 1996 Wilaya ya Kwimba iligawanywa na kuwa Wilaya ya Misungwi na Kwimba ya sasa.
1.1: Mahali ilipo
Wilaya ya Kwimba ipo kwenye latitudo 2o 45’ na 3o 53’ Kusini mwa Ikweta na longitudo 33o na 33o 30’ Mashariki mwa Meridiani. Kaskazini Wilaya imepakana na wilaya ya Magu, Mashariki inapakana na wilaya ya Maswa, Kusini inapakana wilaya ya Kishapu na Shinyanga Vijijini na upande wa Magharibi imepakana na wilaya ya Misungwi.
1.2: Eneo na Maeneo ya Utawala
Wilaya ya Kwimba ina eneo la kilometa za mraba 3,903, ina Tarafa tano (5), Kata 30, Vijiji 119, Vitongoji 871 na Mamlaka ya Mji Mdogo. Pia ina majimbo mawili (2) ya Uchaguzi wa Bunge na Madiwani ambayo ni Kwimba na Sumve. Makao Makuu ya Wilaya ni Ngudu yaliyo umbali wa kilomita 98 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Mwanza.
1.3: Idadi ya Watu.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, wilaya Kwimba ilikuwa na jumla watu 406,509 kati ya hao wanawake 198,096 na wanaume 208,414. Ongezeko la watu kwa mwaka ni 1.9% na ujazo wa watu kwa kilomita za mraba 106. Kwa sasa wilaya inakadiliwa kuwa na watu 462,663 kati yao wanaume ni 237,203 na wanawake 225,460 (makisio ya takwimu ya Taasisi ya Taifa kuishia mwezi Desemba 2016)
1.4: Hali ya Hewa.
Wilaya ya Kwimba kwa sehemu kubwa ni tambarare, mabonde na miinuko michache na vilima vya hapa na pale. Hali ya hewa ya Wilaya hii ni ya ukame kwa ujumla, ambapo mvua ni haba, haziaminiki au kutabirika kwa urahisi. Wastani wa mvua kwa mwaka ni milimita 700-1200. Kiwango cha joto ni nyuzi 250-330C kwa mwaka; na pepo kavu karibu mwaka wote. Majira ya hali ya hewa yamegawanyika katika sehemu kuu tatu yaani majira ya mvua ya muda mfupi (vuli) ambayo huanza katikati ya Oktoba hadi Desemba, majira ya kipindi kirefu cha mvua (masika) ni katikati ya Februari hadi Mei na majira ya kipindi kirefu cha jua ni kati ya Juni hadi katikati ya Oktoba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.