IDARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
Lengo
Kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo ya viwanda, biashara, masoko na uwekezaji. Majukumu Kitengo kitafanya kazi zifuatazo:-
Kuratibu utekelezaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu zinazohusiana na viwanda, biashara, masoko na uwekezaji;
Kukuza viwanda, biashara, masoko na uwekezaji katika Halmashauri;
Kupanga na kuendeleza maeneo ya viwanda na hifadhi kwa kushirikiana na wadau wengine wakuu;
Kupanga vivutio vya viwanda, biashara, masoko na kukuza uwekezaji;
Kukuza maendeleo ya Biashara Ndogo na za Kati (SMEs);
Kuendeleza mapendekezo na miradi ya uwekezaji;
Kuendeleza hatua za maendeleo ya sekta binafsi;
Kuanzisha na kusimamia kanzidata ya viwanda, biashara, masoko na uwekezaji;
Kusimamia usimamizi wa kituo kimoja cha biashara;
Kufanya utafiti wa kukuza uwekezaji;
Kuratibu Jukwaa la Biashara;
Kusimamia shughuli za minada na masoko katika Halmashauri;
Kutekeleza Mkakati wa Maendeleo ya Biashara kwa wafanyabiashara wadogo na watoa huduma; na
Kuweka Mazingira bora ya Biashara na uwekezaji ili kukuza Biashara na Uwekezaji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.