ALAT Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mwenyekiti Mhe.Mpandalume Saimon wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambayo imeanza kutoa huduma za Afya tarehe 21, Februari 2023.
Viongozi hao wametoa pongezi hizo leo Februari 23,2023 wakati wakifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa Wilayani Kwimba
" tuwaponge viongozi wa Kwimba maana mmefanya kazi kubwa sana kukamilisha Hospital Kwa kiwango kikubwa hivi,mmenunua vifaa vya kisasa na mmeshaanza kuvitumia hii nihatua kubwa sana" amesema Mpandaluma
Naye meya wa Jiji la Mwanza amesema wameshafanya ziara Halmashauri nyingi za Mkoa wa Mwanza lakini wengi hawajafikia hatua iliyofikiwa Kwimba Kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
" Ujenzi umekamilika Kwa kiwango, majengo yanavifaa vya kisasa na hii haitoshi mmefungua huduma Kila kitu kikiwa kimekamilika hii ni hatua kubwa sana"
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri ilipokea bilioni 1.05 kwaajili ya kujenga jengo la dharura, jengo la ukunga na wodi mbili majengo yote yamekamilika na fedha iliyosalia imetumika kukamilisha majengo mengine ya Hospitali hiyo ambayo yalikuwa hayajakamilika Kwa kuwekwa milango na madirisha.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.