Naibu Waziri Wizara ya Elimu Mheshimiwa Omary Juma Kipanga amefanya ziara Wilayani Kwimba leo tarehe 23 Julai 2021 kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA.
Katika ziara hiyo Mhe.Kipanga amepongeza juhudi za wahandisi na msimamizi wa ujenzi huo kwa hatua waliyofikia na ubora wa majengo,amewapongeza mafundi wanaoshiriki ujenzi huo pamoja na Jeshi la Magereza kwa ushirikiano wanaoufanya kuhakikisha majengo yote yanajengwa kwakiwango kinachotakiwa.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Kipanga ameahidi kuleta fedha zilizopelea kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Chuo hicho. " tutamaliza ujenzi huu iwe jua iwe mvua iwe usiku iwe mchana naahidi tutamaliza" amesema Kipanga.
Akisoma taarifa ya mradi huo msimamizi wa mradi Mhandisi Juliana Magesa Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kagera. amesema majengo 16 yanajengwa yakiwemo madarasa, mabweni,vyoo,nyumba za watumishi,jengo la utawala,na kalakana.Ambapo jumla ya bilion 1.6 zilipokelewa na zimekwisha tumika na majengo yamefikia asilimia 86 hivyo ameomba kuongezewa kiasi cha milioni 502 ili kukamilisha ujenzi huo.
Aidha Naibu Waziri ametoa rai kwa msimamizi wa mradi huo kuendelea kusimamia fedha za Serikali kwa umakini kwani jukumu la ujenzi wa vyou ni kubwa hivyo usimamizi uongezwe ili vyuo hivyo vilete tija kwa Taifa.
Naibu Waziri amesisitiza watumishi na watu wote wanaoshiriki ujenzi huo kuendelea kuwa wazalendo,waadilifu,waaminifu na wamuogope Mungu wanapofanya kazi za Serikali ili kusitokee udanganyifu wowote katika kazi ya ujenzi.
Ujenzi wa Chuo hicho ulianza Februali 2020 na unatarajiwa kukamilika Septemba 2021 endapo fedha za kukamilisha zitafika kwa wakati
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.