Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba yashauliwa kuhakikisha hoja za miaka ya nyuma zinafungwa na walio sababisha kutokea kwa hoja hizo kutafutwa ili washiriki kujibu na kuondoa hoja hizo.
Hayo yamejiri leo Juni 22, 2022 kwenye kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani lililolenga kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021.
“Hatukubali kulea uzembe popote ilipo fedha ya umma lazima irudi, hata kama aliyekula amehama akatwe kwenye mshahara wake na kama amestaafu akatwe kwenye pensheni yake ili fedha za Serikali zirudi hapa.” Amesisitiza Mkuu wa Mkoa Mhe. Mhandisi Robert Gabriel.
Naye katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Ngusa Samike amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kuweka mikakati itakayowawezesha kuzui kutokea kwa hoja na wametakiwa kujibu hoja zote ili kuondoa mrundikano wa hoja. ”wekeni mikakati mjibu hoja zote ili ziondoke,Mkurugenzi lazima uhakikishe kila Mkuu wa Idara anajibu hoja zake” amesema Ngusa
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mwanza, Waziri Shabani amesema Mwaka 2020/21 Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilikaguliwa na kupata Hati Inayoridhisha na kuanzia mwaka 2012/13 hadi 2020/2021 Halmashauri hiyo ina jumla ya Hoja 120 ambapo 70 zipo kwenye hatua mbalimbali ya Utekelezaji na 50 zimefungwa.
“Mhe. Mwenyekiti, sababu kubwa ya hoja kutofungwa kwenye Halmashauri hii ni kutokana na Halmashauri kutoweka mkakati thabiti wa kujibu Hoja kikamilifu na Menejimenti kutokua na vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha matumizi na malipo mbalimbali yaliyofanyika.” Amesema Shabani
Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa amekagua mradi wa ujenzi wa Kantini ya Halmashauri ambapo ameshauri wasimamizi wa mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike kama ilivyokusudiwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.