"Hapo zamani za kale Pamba iliwahi kuongoza,Kwimba ikatamkwa kwamba ndiyo ilikuwa Wilaya ya Kwanza kuzalisha pamba vizuri, sasa nin kilichotokea?
Maneno hayo yamesemwa na Balozi wa Pamba Mhe. Aggrey Mwanri alipokuwa akitoa elimu ya kilimo bora cha Pamba kwa Maafisa Ugani, Watendaji wa Kata na Vijiji na watumishi wengine wa Halmashauri leo tarehe 05/11/2021 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu.
Katika mafunzo hayo Mwanri amewataka Maafisa hao kwenda kuwa mabalozi kwa kuwafundisha Wananchi namna bora ya kilimo cha pamba ili waweze kupata mavuno mengi na wapate pamba safi.
Amesisitiza kuwa Wakulima wanaolima kwa kufuata utaratibu unaotakiwa wanafanikiwa sana kwani wanaouwezo wa kupata pamba nyingi mara tatu zaidi ya mkulima anayelima kilimo holela.
" Tumekuja kuchaji betri zenu, kuweka pumzi nyingine kwa wanakwimba ili mlime Pamba kisasa, kilimo cha Faida"
amesema Mwanri
Katika mafunzo hayo ameshiriki Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi ambaye amemuahidi Mwanri kufanyia kazi mafunzo aliyoyatoa kwa kuhakikisha Wananchi wanalima Pamba kisasa ili waweze kujiongezea kipato kwa kuzalisha pamba nyingi zaidi ili kuiwezesha Kwimba kurudi kwenye nafasi yake ya kuwa mzarishaji bora wa Pamba.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Bi. Happiness Msanga amewataka Maafisa wote walioshiriki mafunzo hayo kwenda kuwafundisha Wakulima wa pamba ili wanapoanza msimu wa kilimo cha pamba walime kisasa.
Balozi Aggrey Mwanri amedhamilia kuirudisha Kwimba kuwa mzarishaji bora wa Pamba hivyo atapita katika baadhi ya vijiji kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba kwa Wananchi ili atengeneze mabalozi wengine wengi wa zao la Pamba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.