Mheshimiwa Agrey Mwanri Balozi wa pamba Tanzania amewashauri wakulima wa zao la pamba kutokata tamaa ya kulima zao hilo kutokana na bei ya zao hilo kushuka hadi 1050 kwa mwaka huu 2023.
Ameyasema hayo leo Oktoba 4,2023 katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu
"bei ya pamba inapangwa na soko la Dunia ndiyo maana inapanda na kushuka kulingana na uzalishaji, kwahiyo wakulima wasikate tamaa waendelee kulima maana mwaka ujao bei inaweza kupanda" amesema Mwanri
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka Watendaji na Maafisa ugani kwenda kuwa mabalozi kwa wananchi kwa kuwafundisha kulima pamba kwa kuzingatia vipimo na matumizi sahihi ya viuwadudu ili waweze kupata kilo 2000 hadi 2500 kwa hekali moja.
Katika mafunzo hayo ameshiriki Kaimu Mkurugenzi Ananiacy Mbandwa ambaye amewataka Watendaji na Maafisa ugani kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikisha Elimu waliyopata kwa wakulima wa pamba
"kwetu Kwimba pamba ni uchumi kwahiyo tukasimamie na kuhamasisha wakulima walime Pamba na mazao mengine ya biashara" amesema Mbandwa
Naye Afisa Kilimo Wilaya Mhandisi Magreth Kavalo amewaelekeza Maafisa ugani na Watendaji kwenda kuwahamasisha wakulima kung'oa maotea ya pamba yote kabla hawajaanza kupanda zao hilo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.