Baraza la madiwani limeshauri fedha zilizobaki wakati wa ufungaji wa hesabu za Halmashauri 2021/2022 zitumike haraka ili zikamilishe miradi ya maendeleo.
Wameyasema hayo leo tarehe 27,Sept 2022 katika mkutano wa baraza la madiwani la kufunga hesabu za Halmashauri 2021/2022 ambalo limeonyesha kuwa wakati wa kufunga hesabu Halmashauri ilifunga hesabu ikiwa na bilioni 4.2 ambazo zililetwa mwisho wa mwaka kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la utawa,fedha za ujenzi wa vituo vya Afya,fedha za miradi ya TASAF na miradi mingine.
Akisoma taarifa ya ufungaji wa hesabu hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauti ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Msanga amesema mwaka 2020/2021 hesabu zilifungwa na halmashauri ilibaki na bilioni 1.5, tofauti na mwaka 2021/2022 ambapo hesabu zimefungwa na Halmashauri imebaki na bilioni 4.2 ikiwa ni fedha za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa jengo la utawala, vituo vya Afya na miradi mingine.
Mkutano huo umehudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Samizi ambaye amesisitiza ukusanyaji wa mapato ili kuongeza makusanyo yatakayosaidia uanzishwaji wa miradi mingi ya maendeleo.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ameutumia mkutano huo kuwaomba wajumbe wote kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wanawake wajawazito,watoto na watu wengine wenye uhitaji wa damu. Zoezi la kuchangia damu limefanyika hapo Halmashauri ambapo watumishi wengi wamejitoa kuchangia damu.
Akifunga mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Thereza Lusangija amewataka madiwani na viongozi wengine kwenda kuhamasisha ujenzi wa vyoo,ukusanyaji wa mapato,nidhamu na ushirikiano.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.