Madiwani waishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo Wilayani Kwimba.
Wameyasema hayo kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika Mei 19,2023 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
" tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametuletea fedha nyingi za miradi, hii hijawahi kutokea, tumepata miradi ya Elimu na Afya hii imepunguza michango kwa Wananchi ya kuchangia maendeleo sasa mchango unaotoka kwa wananchi ni nguvu kazi kama kuchimba msingi lakini siyo kutoa fedha" amesema Gervas Kitwala
Akiwasilisha taarifa ya robo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri imepokea fedha zaidi ya bilioni 9 Kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya,ujenzi wa madarasa, ukamilishaji wa madarasa. Nyumba za walimu, ujenzi wa Zahanati,ukamilishaji wa Zahanati,ujenzi wa vituo vya Afya, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na ujenzi wa jengo la utawala.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.