Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba likiwa chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Thereza Jackson Lusangija limepitisha kiasi cha bilioni 44.89 kama bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2021/2022.Ikiwa na mchanganuo ufuatao mapato ya ndani bilioni 2.5, mishahara bilioni 29.2, ruzuku ya matumizi ya kawaida bilioni 1.6, ruzuku ya miradi ya maendeleo bilioni 11.5
Akiongea katika ukumbi wa Halmashauri Mhe.Lusangija amesema matarajio ya Madiwani wa Halmashauri nikuona mambo yaliyopangiliwa kwaajili ya kuleta maendeleo ya wananchi wa Kwimba yanafanikuwa kwa kiwango kikubwa,pia amesisitiza kuwa atatumia nafasi yake kuhamasisha na kusimamia miradi na shughuli nyingine zinazochagiza maendeleo zinafanyika ili mipango yote iliyojadiliwa katika bajeti hiyo iweze kufanikiwa.
Katika baraza hilo amehudhuria Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Simon Ngaga yeye amewapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa kupitisha bajeti hiyo pia amewashauri wabuni na kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato ya ndani,vilevile amewasisitiza Madiwani kuwa mstari wa mbele kusimamia miradi inayotekelezwa katika Kata zao ili miradi ikamilike kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.