Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan ameendelea kutoa hamasa katika michezo na kuboresha miundombinu ya michezo.
Katika kutekeleza hilo Wilaya ya Kwimba imepokea bilioni 31 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha michezo ( Sport center) ambapo miundombinu ya madarasa,Hosteli,jengo la Utawala na viwanja vya michezo vimeanza kujengwa.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wakandarasi wa kampuni ya CRJE wanaotekeleza mradi huo kuhakikisha wanazingatia ubora na thamani ya fedha
" nimefurahi kuona mradi umeanza na kasi inatia moyo endeleeni kuongeza kasi tuendelee kumtia moyo Mheshimiwa Rais anayetoa fedha kwaajili ya kutekeleza mradi huu akilenga kuboresha michezo pia hakikisheni mnazingatia ubora na thamani ya fedha"amesema Ludigija
Baada ya kukagua mradi huo Ludigija amefungua mafunzo maalum ya michezo ( special Olympics) yanayofanyika chuo Cha Michezo Malya ambayo yamelenga kuboresha ufundishaji wa michezo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
" Kama mnavyojua michezo ni ajira michezo ni Afya tumieni mafunzo mtakayopata kwenda kuwafundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, zingatieni kuwa nao wanahitaji kushiriki michezo mbalimbali hivyo tumieni elimu mtakayopata kuifikisha kwao"
Nao wanafunzi wa chuo hicho wakiwakilishwa na Ladislaus Lunguya wameushukuru uongozi wa chuo hicho kwa kuleta mafunzo maalum na wameahidi kwenda kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum kufikia ndoto zao katika michezo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.