Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amevitaka vyombo vya watoa huduma za maji ngazi ya jamii( CBWSO) kuhakikisha wanaongeza Mtandao wa maji ili kuwafikia Wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma hiyo.
Ameyasema hayo leo Oktoba 30,2023 katika Mkutano Mkuu wa vyombo vya watoa huduma za maji ngazi ya jamii " sitokubaliana Wala kuivumilia CBWSO itakayoshindwa kuongeza Mtandao wa maji, CBWSO inayokusanya hela na kujilipa bila kuongeza Mtandao itachukuliwa hatua za kisheria" Ludigija
Mkuu huyo amesisitiza kuwa viongozi wa CBWSO wanatakiwa kuwa wabunifu kuanzisha miradi itakayowawezesha kukusanya fedha nyingi zitakazosaidia kuendeleza miradi na kuongeza Mtandao wa maji.
Aidha viongozi wa CBWSO wametakiwa kutumia mfumo ulioanzishwa na wizara ya maji wa ukusanyaji wa fedha ambapo fedha za maji zitalipwa kwa kutumia kumbukumbu namba ambapo kupitia mfumo huo wahasibu hawatatakiwa kupokea fedha kutoka kwa wateja.
Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kwimba Mhandisi Godliver Gwambasa amewashauri viongozi wa CBWSO kushirikiana na kubadirishana ujuzi ili kuboresha huduma za maji vijijini.
Viongozi wa CBWSO wameahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo na ushauri uliotolewa na viongozi walioshiriki mkutano huo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.