Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Simon Ngaga akifungua mafunzo ya Madiwani tarehe 13/01/2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Kwimba amewaasa Madiwani kuzingatia mafunzo wanayopewa ili yakawasaidie kusimamia utaratibu utakaoleta maendeleo katika Kata zao,amesisitiza kuwa wananchi wanaimani na Serikali kutokana na mazuri yaliyofanyika awamu iliyopita hivyo Madiwani wameaswa kwenda kuyaendeleza mazuri yote.DC amewaasa Madiwani kwenda kufanya kazi kwa weredi na kuhamasisha wananchi kufanya kazi za maendeleo na amewataka wakawashauri wananchi kujiunga na bima ya Afya iCHF iliyoboreshwa ili wawe na uhakika wa matibabu kwani Afya bora ndio mtaji.
Aidha DC amesema Halmashauri ya Kwimba imejiandaa kupokea wanafunzi wote wa kidato cha kwanza, meza, viti na madarasa vimeshaandaliwa na vichache vinaendelea kuandaliwa hivyo wanafunzi wote wanaendelea kupokelewa katika Shule walizopangiwa na amesisitiza kuwa 'hakuna Mwanafunzi atakaye somea chini ya mti'. Ameongeza kuwa Halmashauri imeanzisha Shule mpya za Sekondari nne ambapo Shule mbili yaani Shilembo na Hungumalwa ziko tayari kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza,vilevile amesema Halmashauri inamikakati ya Kujenga Shule ya Sekondari ya wasichana ya Wilaya ili kukabiliana na changamoto wanazopata wanafunzi wa kike.
Katika tukio hilo Mhe. Ngaga ametoa hati za viwanja kwa wananchi ambao hati zao zilikua tayari na amemshauri Afisa Ardhi kujitahidi kuandaa hati nyingi zaidi kulingana na maelekezo ya Wizara.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.