Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Samizi ameahidi kuwachukulia hatua wote watakaothibitika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi. Ameyasema hayo leo tarehe 9/9/2020 kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu wakati akifanya uzinduzi wa miongozo ya Elimu
“ ikithibitika unafanya mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi au umempa mimba mwanafunzi sikuachi lazima ufungwe tu, na hapa tuelewane walimu wapendeneni wanafunzi,waleeni na kuwatunza kama watoto wenu, Mwalimu atakayethibitika anamahusiano ya kimapenzi na Mwanafunzi atafungwa hili nitalisimamia” amesema Samizi
Aidha Mkuu huyo amewataka Maafisa Elimu kuweka mikakati itakayowasaidia wanafunzi kufanikiwa katika masomo yao ikiwa ni pamoja na kubadiri mfumo wa masomo yaani wanafunzi wakienda Shuleni wasome hadi saa nane kisha warudi nyumbani, siyo kwenda na kurudi kama ilivyo sasa kitu kinachopelekea wanafunzi wengi kuchoshwa na safari ya kwenda na kurudi hivyo kupelekea wanafunzi wengi kuwa watoro na wengine kuacha masomo
Miongozo hiyo iliyozinduliwa ni mwongozo wa uteuzi wa viongozi wa Elimu,mwongozo wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa Elimu Msingi na mwongozo wa changamoto katika uboreshaji wa Elimu Msingi na Sekondari. Miongozo hiyo imelenga kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokamilisha mzunguko wa Elimu na kukabiliana nachangamoto zinazohafifisha malengo ya wanafunzi.
Walimu walioshiriki uzinduzi huo wameahidi kwenda kufanyia kazi miongozo hiyo na kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.