Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Simon Ngaga amefanya kikao na wafanyabiashara wa Choroko leo tarehe 03/02/2021 na kuwataka kufanya biashara hiyo kwa kuzingatia utaratibu na sheria zilizowekwa na Serikali.
Mkuu wa Wilaya amefanya kikao hicho ili kuwapa maelekezo ya Serikali kuhusu uuzaji wa choroko, amesisitiza kuwa Serikali imeamua kuweka utaratibu wa kuuza Choroko kwa njia ya mnada chini ya vyama vya ushirika (AMCOS) ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa zao hilo.Vilevile amewashauri wafanyabiashara hao kufuata utaratibu huo wakati mapendekezo yao yakipelekwa ngazi za juu.
Amesisitiza kuwa kikao hicho hakikuwa cha kubadirisha utaratibu wowote wa Serikali hivyo watakaokiuka utaratibu huo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kutaifishwa mzigo utakaokamatwa,amesema "sitabadirisha utaratibu wa Serikali Choroko zitaendelea kuuzwa kwa mnada chini ya vyama vya ushirika na tutakayemkamata anatorosha Choroko tutamchukulia hatua kali ikiwemo kutaifishwa mzigo utakaokamatwa"
Wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho wameomba maoni yao yafanyiwe kazi ili waweze kuruhusiwa kufanya biashara hiyo kwa utashi waliouzoea, wamesema wako tayari kulipa ushuru wote wa Halmashauri na AMCOS ila tu waruhusiwe kuuza Choroko mahali wanapotaka wao bila kuhusisha mnada na vyama vya ushirika.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.