Mhe: Senyi S.Ngaga Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amekabidhi vitabu 5345 na vifaa vya maabara kwa Wakuu wa shule zote za sekondari za Wilaya ya Kwimba. Katika Hafla hiyo DC amemshukuru Raisi wa Tanzania Dkt.John Joseph Magufuli na Wizara ya elimu kwa kuuona umuhimu wa kuleta vitabu na vifaa vya maabara katika Wilaya ya Kwimba.Aidha DC amewasisitiza wanafunzi waliokuwepo kama wawakilishi wa wanafunzi wote kusoma kwa bidii na kuvitumia vitabu na vifaa hivyo vilivyotolewa ili vilete manufaa katika elimu yao kwa kuwaongezea ujuzi na maarifa,pia amewataka wanafunzi hao kuitunza miundombinu ya shule zao vizuri ili idumu kwa kipindi kirefu.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bib.Pendo Malabeja ameishukuru serikali kwa kuleta vitabu na vifaa vya maabara na akasema vitabu hivyo vitatumika kuongeza ufaulu,pia amesisitiza kuwa kupitia vitabu hivyo vitasaidia kutokomeza ziro katika Wilaya hii.
Afisa Elimu wa Sekondari Mwalimu Emmanuel Katemi akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi amesema vitabu hivyo vilivyoletwa vitasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa mitihani ya ndani na mitihani ya Taifa,ufauru utakaoongeza ari ya wanafunzi kupenda masomo hasa ya sayansi.Vitabu 5345 vilivyokabidhiwa ni vya masomo ya History 2234 na Geography 2234 kwa kidato cha kwanza na cha pili, Bam 65,Biology 82,Chemistry 220, Kiswahili 368, Physics 92 kwa kidato cha tano.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.