Mhe:Senyi Ngaga Mkuu wa Wilaya ya Kwimba akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama,kaimu mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari wamekagua maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Tallo.Shule ya sekondari Tallo imechaguliwa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu ambapo inatarajia kupokea wanafunzi wa kiume 80 wa tahasusi za EGM na HGK.
Katika ziara hiyo Mhe: Ngaga ameshauri tatizo la upatikaji wa maji litafutiwe ufumbuzi haraka ili wanafunzi wasitumie muda mrefu kufuata maji kwa ajili ya matumizi yao,hii imetokana na kisima kuwa mbali kidogo na mazingira ya shule.Pia Mhe:Ngaga ametembelea karakana mbalimbali zinakotengenezwa samani za wanafunzi ikiwemo viti na meza,vitanda na meza za bwaloni.
Aidha DC ameshauri bweni moja kupewa jina la Mhe:Richard Ndasa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Sumve ili iwe kumbukumbu ya kile alichokifanya wakati wa uhai wake kufanikisha upatikanaji wa mabweni hayo kwa ajili ya kuanzisha kidato cha tano na sita.
Mkuu wa shule hiyo Mwalimu:Fadhili Yusufu amesema "tunaendelea na maandalizi ya vifaa na mazingira kwa ujumla ifikapo tarehe 16,Julai 2020 tunatarajia vifaa vyote vya bwenini na darasani vitakua vimeshakamilika,baadhi ya vifaa kama vitanda vimeshafika na vingine viko hatua ya kumalizika".Aidha Mwalimu Fadhili ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri wote aliopewa na viongozi hao ili wanafunzi watakapofika shuleni hapo kilakitu kiwe kimekamilika kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.