Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi S.Ngaga amewataka watumishi wasioweza kufanya kazi kwa kasi ya awamu ya tano wajiondoe kwenye Utumishi ili wawekwe watu waliotayari kufanya kazi,DC ameyasema hayo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya kilichofanyika jana tarehe 15/12/2020 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Kwimba.
Katika kikao hicho wakuu wa Idara na viongozi wa Taasisi mbalimbali waliweza kuwasirisha Taarifa zao za miradi ya maendeleo.Akiwasirisha taarifa yake Meneja wa TARURA Eng Dickson L.Mwangwa amesema Serikali inayo mikakati ya kufungua barabara mpya,kukarabati barabara mbovu na kutengeneza madaraja ili kuondoa adha wanayoipata wananchi pindi mvua zinaponyesha baadhi ya madaraja yanafurika maji.Pamoja na hayo wajumbe wakataka kujua mkakati wa Serikali kuhusu Kujenga barabara ya rami ya kutoka Hungumalwa- Ngudu- Magu, hapo Katibu Tawala wa Wilaya Ndug. Ally Nyakia akajibu kuwa Serikali imeshafanya upembuzi yakinifu na wakati wowote barabara hiyo itajengwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bib.Pendo Malabeja
Meneja TARURA Eng. Dickson Mwangwa
Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Malya Ndug. Frank Josephat
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya Ndug. Frank Josephat akatumia nafasi hiyo kuwaomba wajumbe wa kikao kukitangaza Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya kuwa ni chuo cha Serikali na kinatoa mafunzo ya ufundi umeme,ufundi bomba,ushonaji,ufundi wa magari(makenika) na Elimu ya Sekondari kwa wasichana waliokatizwa ndoto za kusoma kwa kupata mimba,kulazimishwa kuolewa na sababu nyingine wanasomeshwa bure,pia Mkuu wa Chuo amewaomba wananchi wote wenye vijana waliohitimu kidato cha nne na ambao hawakusoma Sekondari wote kwenda kusoma Chuoni hapo kwani kila mtu anapata mafunzo kulingana na kiwango chake cha Elimu.
Katika kikao hicho kiongozi wa Shirika la Reli Wilaya ya Kwimba amewashauri wananchi kutumia usafiri wa treni kwani treni ya mwendo kasi inakaribia kuanza kujengwa inayopita Wilayani hapa na kwa bahati mzuri kutakuwa na Kituo kikubwa (station) hapa Wilayani Kwimba eneo la Nkalalo (Bukwimba) na Kituo hicho kitakuwa cha abiria na mizigo hivyo amewataka abiria na wafanyabiashara wote kuwa tayari kutumia usafiri huo.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wajumbe wa kikao hicho kuwa maendeleo ya Wilaya hii hayataletwa na watu wengine bali ni wananchi wote na viongozi kila mtu akitimiza wajibu wake Wilaya ya Kwimba itasonga mbele sana.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.