Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Johari Samizi ameshauri viongozi wa dini watumike kufikisha elimu mbalimbali ikiwemo umuhimu wa chanjo ya polio kwa watoto.
Ameyasema hayo leo tarehe 30, Nov 2022 kwenye kikao cha kamati ya Afya kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri. Amesisitiza kuwa viongozi wa dini wanayonafasi ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi.
“tuwatumie viongozi wa dini kufikisha hii elimu ya umuhimu wa chanjo ya polio ili iwafikie wananchi wote kwa wakati hii itatusaidia kufikia watoto wengi na hivyo kuwakinga na ugonjwa wa kupooza”
Chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano itaanza kutolewa kuanzia tarehe 1- 4 Disemba 2022, hivyo wananchi wote wenye watoto wenye umri huo wanatakiwa kuchanjwa ili kukingwa na ugonjwa wa kupooza.
Katika kikao hicho wameshiriki viongozi kutoka wizara ya Afya, TAMISEMI na Afisa kutoka shirika la Afya Duniani (WHO) .AidhaDaktari Gerlad Maro kutoka WHO ameshauri elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili watambue umuhimu wa chanjo hiyo kwa watoto.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.