Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka watumishi wa Idara ya Afya kufanya kazi kwa upendo huku wakizingatia sheria na taratibu zinazoongoza kazi zao. Ameyasema hayo leo April 14,2023 wakati akifanya kikao kazi na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba
" Wahudumieni wagonjwa kwa upendo, wagonjwa wote wanatakiwa kupata huduma sawa kwahiyo zingatieni sana huduma kwa wateja mnazitoa inavyotakiwa au unamuhudumia mtu akitoka hapo anakwenda kusema Icheja hapafai kabisa!, tena wale wachache mnaotoa huduma mbovu badirikeni tunataka kuona wagonjwa wanaipenda hii hospitali, wagonjwa waje kutoka hata nje ya Wilaya wafuate huduma nzuri zinazotolewa Kwimba" amesema Ludigija
Aidha Mkuu huyo amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa kupendana na kusaidiana Ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora zaidi.Pia amewasisitiza watumishi hao kutimiza wajibu wao kwa kufika Hospitali kwa wakati na kuzingatia taratibu zote zinazotakiwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa.
Mkuu huyo amewasisitiza watumishi hao kutumia lugha nzuri wanapotoa huduma kwa wagonjwa ili kuongeza chachu ya wagonjwa kupenda kutibiwa na kupata huduma hospital
"mawasiliano ya dakitari au muuguzi na mgonjwa yanaweza kuongeza ugonjwa au kupunguza ugonjwa kwahiyo zingatieni mawasiliano mazuri na wagonjwa.
Vilevile Mheshimiwa Ludigija amekemea tabia ya kuomba au kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa " kama Kuna baadhi yenu mnaomba chochote kwa wagonjwa ndipo muwahudumie acheni hiyo tabia, tabia hiyo haikubariki na hatutaivumilia yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria" Ludigija
Katika kikao hicho ameshiriki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga ambaye amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zinazoongoza utumishi wa umma.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.