Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Saimon Ngaga amefanya uzinduzi wa madarasa mawili na bwalo kwa ajili ya uanzishwaji wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Tallo.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Yusufu Fadhili akisoma risala amesema shule ya Tallo ina jumla ya wanafunzi 566 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tano ambapo kidato cha tano ndio kimeanzishwa mwaka huu na jumla ya wanafunzi 56 wamesharipoti.Akielezea maandalizi yaliyofanyika kwa ajili ya kuanzisha kidato cha tano Mkuu wa Shule amesema jumla ya milioni 250 zimetumika kuandaa miundombinu ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili,ukarabati wa bwalo,ujenzi wa jiko,ujenzi wa madarasa mawili,ujenzi wa vyoo,na ununuzi wa vitanda,meza za chakula na meza na viti vya kusomea.
Mkuu wa Wilaya akiongea na watu waliohudhuria kwenye hafla hiyo amewataka wanafunzi hao wa kidato cha tano kusoma kwa bidii ili lengo liweze kutimia,pia amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wa maandalizi ya upokeaji wa wanafunzi hao.Aidha Mhe Ngaga ameongelea Taifa limefikia uchumi wa kati hivyo wanafunzi wanatakiwa wasome ili kuondoa ujinga kwani hatuwezi kuimarisha uchumi wa kati kama nchi itakua na wajinga amesema serikali inatoa fedha nyingi katika idara ya elimu ili wanafunzi wasome bila matatizo.Pia Mkuu wa Wilaya amesema serikali imefanya miradi mingi ya maendeleo katika wilaya ya Kwimba hivyo wananchi tuitumie miradi hiyo kutuletea maendeleo ili tuendane na uchumi wa kati.
Afisa Elimu Sekondari amemshukuru DC kwa kufika katika hafla hiyo na ameahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya na ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta fedha za kuboresha miundombinu ya shule katika Wilaya ya Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.