Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi S.Ngaga amezindua ofisi ya Sungusungu kijiji cha Nyang'honge,jengo hilo lina vyumba viwili vya ofisi na kaukumbi kadogo kwaajili ya vikao.Katika uzinduzi huo DC amekagua boma la darasa na ofisi ya walimu ambalo limejengwa na jeshi hilo la sungusungu katika shule ya Msingi Nyang'honge.pia amewashauri wananchi wote kupeleka watoto wao shule na kuhakikisha wanafunzi wanasimamiwa ili kumaliza masomo yao na kuongeza idadi ya wasomi katika kijiji chao ili kuongeza chachu ya maendeleo.
Katika sherehe hiyo imefanyika harambee kwaajili ya umaliziaji wa jengo hilo la darasa na ofisi ya walimu ambapo kiasi cha milioni tano kimepatika,DC na msafara alioongozana nao amewaahidi bati na vifaa vingine vya thamani ya milion mbili, wananchi na vikundi mbalimbali vya sungusungu wamechangia fedha taslim milion tatu.
DC akiwahutubia wananchi wa kijiji hicho amelipongeza jeshi hilo la sungusungu kwa kuona umuhimu wa kujenga darasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Nyang'honge kwani wanafunzi watakao anza darasa la kwanza mwaka ujao hawatapata changamoto kwani wana vyumba vya kutosha kulingana na idadi ya wanafunzi walionao.Pia DC amelipongeza jeshi hilo la Sunguaungu kwa kujenga ofisi yao kwani itarahisisha upatikanaji wao.Pamoja na hayo DC amewashauri sungusungu hao kuanzisha mradi utakaowaongezea kipato katika kikundi chao.
Aidha DC amewashauri wnanchi wa kijiji hicho kujenga nyumba bora za tofali za kuchoma na bati ili kuongeza maendeleo katika kijiji hicho, amesema "tuhakikishe kwenye senta zetu tunaondoa nyumba za nyasi ili tunapoletewa umeme tuwe kwenye nyumba nzuri na bora , kuna watu wana ng'ombe 100 hadi 500 lakini wanaishi kwenye nyumba za nyasi,tuuze ng'ombe chache tujenge nyumba bora na nzuri za kisasa"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.