Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Mussa Samizi amewaelekeza viongozi wa kijiji cha Igumangobo kubomoa sehemu ya ukuta uliojengwa kwa tofari zisizo na ubora. Haya yamejitokeza jana tarehe 12.Agosti 2021 Kijiji cha Igumangobo Kata ya Mwamala ambapo Mheshimiwa Samizi alikuwa akifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika tarafa ya Mwamashimba.
Mkuu huyo ametoa maelekezo hayo baada ya kukagua jengo la Zahanati na kugundua baadhi ya tofari za jengo hilo hazina ubora unaotakiwa kulingana na vigezo vinavyotolewa na wataalamu.
" kama mkono wangu unamomonyoa tofari basi hili tofari halifai mnataka hili jengo liwaangukie watu? huu upande uliojengwa na haya matofari mabovu ubomolewe" amesema Johari
Aidha Mkuu huyo amesisitiza majengo yote yanayojengwa Wilaya ya Kwimba hata kama wanaojenga ni Wananchi kwa nguvu zao lazima wazingatie maelekezo ya Wahandisi ili majengo yaendane na ubora unaotakiwa ili kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na majengo yasiyo na ubora.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ametembelea Kata zote za Tarafa ya Mwamashimba na kuongea na viongozi wa maeneo hayo, amewasisitiza viongozi kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ya kazi na kuwa wawazi kwa wananchi ili wananchi wafahamu miradi inayotekelezwa na Serikali vilevile amewahimiza viongozi hao kuwasomea wananchi mapato na matumizi ili Wananchi wajue kila kinachoendelea katika vijiji vyao.
Mkuu huyo amewataka viongozi wote wa vitongoji,vijiji na kata kuhakikisha wanaanzisha Benki ya matofari ya kuchoma ili kuweza kukabiliana na upungufu wa miundombinu mbalimbali unapojitokeza.Amewataka kila kijiji kuanza na matofari yasiyopungua 100,000.Vilevile amewasisitiza Wataalamu ngazi ya vijiji na Kata kuendelea kuboresha huduma wanazozitoa kwa jamii.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.