Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Arch.Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija Leo Februari 6,2023 amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Johari Samizi ambaye amehamishiwa Wilaya ya Shinyanga.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mhe. Samizi amewashukuru viongozi wote na wananchi Kwa ushirikiano waliompatia kipindi cha uongozi wake hapa Kwimba,pia ameshauri kasiya usimamizi wa miradi iliyokuwa inatumika iendelee ili Kwimba isonge mbele zaidi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ludigija amewaomba wananchi na viongozi wote kumpa ushirikiano Ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya Kwimba.
Aidha amesisitiza suala la ushirikiano, uwajinikaji na kujituma katika kufanya kazi Kwa watumishi wa umma
" Mimi napenda matokeo kwahiyo niwaombe Kila mtu kwa nafasi yake tufanye kazi tuibadirishe Kwimba, Kwimba ni Wilaya kongwe sana lakini bado tuko nyuma ukilinganisha na Wilaya jirani kwahiyo tupambane kuiinua kiuchumi.Vilevile Kwa kipindi nitakachokuwepo Kwimba Kila mwananchi atatakiwa kuwa na shamba la Pamba lisilopungua heka moja, tunataka tulitumie zao hili kuinua uchumi wa familia, Halmashauri na Taifa kwaujimla" Ludigija
Wakuu wa Wilaya hao wamemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini katika utumishi wao na wameahidi kutomwangusha katika utendakazi wao.
Katika makabidhiano hayo wameshiriki viongozi mbalimbali ambao wamempongeza Mkuu wa Wilaya anayeondoka Kwa ushirikiano aliokuwa anauonyesha katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo na wamemkaribisha Mkuu aliyekuwa na kuahidi kushirikiana naye.
" tunakushukuru sana Mheshimiwa Johari Kwa ushirikiano uliotupatia hivyo tunakuombea na huko unakokwenda ukauendeleze, wewe ni mwanakwimba na tutaendelea kushirikiana na wewe hata ukiwa huko Shinyanga " amesema Mhe. Sabana Rushu Mwenyekiti CCM Wilaya
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.