Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Mussa Samizi leo tarehe 18,Mei 2022 amefanya uzinduzi wa Chanjo ya polio kwa watoto wenye miaka sifuri hadi mitano, uzinduzi huo umefanyika katika maeneo tofauti ya Tarafa ya Mwamashimba.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amepata fulsa ya kuwapatia watoto matone ya chanjo ya polio katika Zahanati ya Kikubiji na Kituo cha Afya Mwamashimba. Pia mkuu huyo ametembelea kaya mbalimbali za Wananchi wa Mwashimba ili kukagua utekelezaji wa utoaji wa Chanjo za polio.
Kampeni hii ya utoaji wa Kinga tiba ya polio imeanza leo hadi tarehe 21 Mei, 2022. Zoezi la utoaji wa kinga linafanyika Nyumba kwa Nyumba ambapo wahudumu wa Afya wanapita kutoa kinga hizo, vilevile kinga hizo zinatolewa katika Zahanati na Vituo vya Afya
Aidha katika kuhakikisha Elimu inawafikia wazazi kwa wingi Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amefika Shule ya Msingi Kikubiji na kuongea na Wanafunzi wa Shule hiyo ambapo amewataka kwenda kuwa mabalozi ili ujumbe huo wa kinga kwa watoto uwafikie wazazi wote ili wawe tayari kuwatoa watoto wao kupata kinga.
Akiongea na Wanafunzi hao Mheshimiwa Samizi amesema madhara ya watoto kutopata kinga ya polio ni makubwa kwani ugonjwa wa polio hauna tiba na ukishampata mtoto anapooza na kupelekea ulemavu.
"waambieni wazazi wenu wawapeleke wadogo zenu kupata chanjo ya polio ili wawaepushe na madhara yanayoweza kujitokeza hasa ugonjwa wa kupooza, tena wasisitizeni kuwa ugonjwa wa polio hauna dawa kwahiyo mtoto akiupata ni hatari kubwa kwake na kwa watoto wanaomzunguka" amesema Samizi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.