Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka watumishi na waheshimiwa Madiwani kutumia mafunzo ya maadili kuongeza uadilifu. Ameyasema hayo leo Juni 20,2023 wakati akifungua mafunzo ya maadili kwa viongozi na watumishi wa umma yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
"mtumie nafasi hii ya mafunzo kuuliza maswali yatakayowasaidia kujijenga,lakini mtambue kuwa uadilifu na utumishi uliotukuka ni vitu ambayo havitenganishwi kwahiyo naamini mkipata haya mafunzo yawasaidie kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria za utumishi" Ludigija
Mkuu huyo amesisitiza Elimu hiyo itumike kuboresha mambo mbalimbali katika Halmashauri na isaidie kila mtumishi kujua mipaka yake katika utumishi. Aidha Mheshimiwa Ng'wilabuzu amewapongeza waandaaji wa mafunzo hayo kwani yataongeza Chachu ya uwajibikaji.
Wakiwasilisha mada mbalimbali wawezeshaji( Innocent Shetui,na Christian Kapele) kutoka Sekretarieti ya Maadili ya utumishi wamesisitiza viongozi na watumishi kujiepusha na mgongano wa maslahi, kuzingatia sheria ya maadili, wajibu wa viongozi, kukuza na kuzingatia maadili mahali pa kazi na katika Jamii.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.