Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wazazi kuongeza uangalizi wa watoto Ili kuwalinda na madhara yanayosababishwa na mmomonyoko wa maadili, pia amekemea ukatili Kwa watoto unaofanywa na baadhi ya watu wasio na maadili
" Kwimba sisi siyo kisiwa kwimba tuna watoto wanaofanyiwa ukatili wa kingono, wengine wanabakwa na kupata mimba ukatili huu haikubariki, tutapambana na mtu yoyote anayefanya ukatili kwa watoto" Ludigija
Katika maadhimisho hayo wadau mbalimbali wameshauri wazazi kuwa karibu na watoto wao Ili kugundua mabadiliko kwa watoto
" tuwalinde watoto wetu, hata wale ambao ni walemavu tusiwaache tu, tuwakinge na unyanyasaji" Julias
Watoto nao hawakubaki nyuma wameiomba Serikali kuendelea kuwalinda dhidi ya ukatili na unyanyasaji ambao baadhi yao wanafanyiwa " tunaiomba Serikali iendelee kutulinda na ukatili,kunawengine wanafanyiwa ukatili nyumbani kwao na wengine shuleni" Enock Mayunga
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu inayosema zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidijitali
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.