Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ngw’ilabuzu Ndatwa Ludigija Leo Februari 3,2023 akiripoti Wilayani Kwimba amemkuta Balozi wa Pamba Mheshimiwa Agrey Mwanri akitoa semina za umwagiliaji wa viuwadudu vya Pamba hapo akatoa neno Kwa washiriki wa mafunzo hayo ambao walikuwa ni watendaji wa Kata na vijiji , wakulima wa mfano, maafisa ugani, viongozi wa AMCOS na wataalamu kutoka Halmashauri.
“ Mimi ni mkulima mzuri sana na hapa Kwimba ni nyumbani kwahiyo niwaombe wanakwimba tulime kilimo cha kisasa chenye tija tena siyo kilimo cha mazao ya chakula tu!, tulime na mazao ya biashara angalau zao moja la biashara hasa Pamba Ili kupitia zao hilo tuinuke kiuchumi tuendelee zaidi ya hapa tulipo” amesema Ludigija
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema anawataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi kama Agrei Mwanri Ili Kila mwananchi ahamasike kulima kilimo bora tena kilimo kitakachoifanya kwimba inabadirika, vilevile amewataka wananchi kutoa ushirikiano Ili kufanikisha malengo ya kuiendeleza Kwimba.
“ hiki ni kipindi cha kumwagilia dawa za kuuwa wadudu, tukifanikiwa hapa tutakwenda mbele zaidi maana tunataka zao la Pamba liwe ndio zao la biashara namba moja hapa Kwimba Ili hata viwanda vilivyokuwa vinaanza kupotea vianze kazi tena” Ludigija
Katika semina hiyo Balozi wa Pamba Mheshimiwa Agrey Mwanri amewataka viongozi na wataalamu walioshiriki semina hiyo kwenda kufikisha elimu ya umwagiliaji wa viuwadudu Kwa wananchi Ili kusaidia kupambana na wadudu wanaoshambulia Pamba.
“ nendeni mkawe mabalozi tunataka kupambana na hawa wadudu wanaoshambulia Pamba, vilevile wafikishieni taarifa wananchi kuwa mwezi wa Saba tutapita kukagua kama maotea yote ya Pamba yameng’olewa, watakaokutwa bado hawajayatoa Sheria zitachukuliwa dhidi yao” Mwanri
Mheshimiwa Mwanri atafanya ziara ya siku tatu hapa Kwimba ambapo anatarajia kupita vijijini kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba hasa namna bora ya umwagiliaji wa viuwadudu vinavyoonekana kuwa tishio Kwa zao la Pamba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.